LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATAKIWA KUPATA MAFUNZO JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA KEMIKALI NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Wafanyabishara  wa  kemikali nchini wametakiwa kupata mafunzo juu ya matumizi sahihi ya kemikali  kabla hazijaleta madhara.

Mkemia  Mkuu wa serikali,  Profesa Samwel Mnyele, alitoa rai hiyo  katika mkutano uliowakutanisha wadau wanatumia kemikali hizo wakiwemo wafanyabishara kutoka taasisi mbalimbali zinazojihusisha na usafirishaji   wa kemikali.

Alisema kumekuwepo na ajali nyingi zinazohusiana na kemikali zinatokana na kutokuwa na uelewa juu  ya madhara yakemikali hizo .

Aidha amesema kuwa kemikali nyingi  zimekua zikileta madhara makubwa kwa watumiaji  na kwamba hali hiyo inachangiwa na wafanyabishara wa bidhaa hizo kutokuwa na uelewa wa namna ya usafirishaji na uhifadhi wa kemikali hizo  huku changamoto kubwa ikielezwa kuwa ni wananchi  kutumia kemikali ambazo zina asili ya kulipuka na kuleta madhara.

Mmoja wa wafanyabishara wa kemikali kutoka kampuni Nabaki Afrika, Josephu Masayo, alisema mafunzo hayo yatawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ikiwemo kuhifadhi na kutunza kemikali katika hali ya usalama.

No comments:

Powered by Blogger.