LIVE STREAM ADS

Header Ads

Usajili wa MeTL Career Fair (Job Bonanza) kufungwa leo jumamosi changamkia fursa.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Displaying Careers fair 2 (1).jpg
Usajili wa MeTL Career Fair (Job Bonanza) kufungwa leo jumamosi changamkia fursa. 

Kama wewe ni mhitimu katika Uhandisi au Utawala (Masoko, Mahusiano, Fedha) na una ari ya kujifunza, ukiwa na mtazamo chanya wa mafanikio na mfuatiliaji wa maadili katika kazi, njoo ujiunge nasi katika bonanza hili la uchambuzi wa ajira.

Rasilimali Watu
Mauzo
Uhasibu
Masoko
Uhandisi
Kilimo
Nguo

Kwani unaweza ukawa mmoja kati ya watu 25 tutakao wachagua kwa ajili ya kujiunga kwenye programu ya uendelezaji wa wahitimu wa vyuo vikuu.

Na ukibahatika kuwa mmoja wapo kati ya hao utapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo katika viwanda vyetu vilivyopo maeneo mbalimbali.

Pia utapata nafasi ya kufundishwa mifumo ya uendeshaji wa viwanda vya kisasa.   
                   
Utakuwa chini ya wakufunzi waliobobea katika kazi zao duniani ambao  watakuwezesha wewe kukua katika kazi na kushika nyadhifa kwenye kazi yako. Zaidi ya yote hayo utakayofanyiwa pia utalipwa ili kujifunza

No comments:

Powered by Blogger.