LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAONI YA MSOMAJI KUFUATIA SAKALA LA MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA NA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akihojiwa na jana na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza, kuhusiana na sakata la Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza kugoma kukabidhi mihuri yao ya utendaji kazi.

Hapo inahitajika mtazamo mpana katika hilo, kama ishu ya kuwanyang'anya mihuri inatokana na uuzaji wa maeneo ya ardhi kiholela, basi waelimishwe juu ya sheria ya ardhi inasemaje katika hilo, kwan tofauti na hapo itasababisha mvutano mkubwa usio na tija wakati sheria zipo wazi katika hilo.

Kuna faida nyingi za kuwanyang'anya mihuri wenyeviti kama hilo la kuwafanya wasiuze maeneo kiholela lakini lazima tuangalie upande wa pili wa shilingi ambapo

1. Wenyeviti wanachaguliwa na wananchi kutokana na namna (sio wote) walivyo msaada mkubwa kwa jamii zinazowazunguka, mara nyingi hekima, jitihada na harakati za kuwatetea watu katika jamii zao hufanya wengi wachaguliwe kuongoza watu wao katika mitaa, sidhan kama hili linaweza kuwa rahisi kwa mtendaji ambaye ameletwa tu katika jamii kwa haraka haraka akaweza kuyasimamia haya

2. Wenyeviti kwa mihuri yao ndio wanaowaandikia barua za dhamana watu wao wanapotuhumia na kesi za jinai kwenda polisi na mahakamani kwa kuwa wanawajua vyema wahusika na mienendo yao katika jamii, sidhan kama hili linaweza kwena vyema kwa watendaji pekee ambao hawawajui wananchi wa eneo husika kwa ukaribu zaidi kama wanaweza kulifanya hili kwa uhakika.

3. Waajiri wengi siku hizi hasa sekta binafsi wanapotaka kumwajiri mfanyakazi lazima wamwombe barua ya udhamini iliyosainiwa na mwenyekiti wa mtaa (sio mtendaji) na picha za mdhamini na mdhaminiwa. Je utaratibu wa kuwanyang'anya mihuri wenyeviti wa mtaa hauwezi wakosesha vijana wengi ajira katika sekta binafsi kutokana na huo utaratibu kuwa unatumika na waajiri wengi hata hapo mwanza.

3. Inawezekana kabisa kwa mtendaji akawa anaishi eneo tofauti kabisa na mtaa anaofanyia kazi (kitu ambacho sio rahisi kwa mwenyekiti kuchaguliwa mtaa asioishi) na mara nyingi inaweza kutokea dharula hata baada ya masaa ya kazi kama vile mwanafunzi anatakiwa asainiwe fomu za mikopo ya elimu, maombi ya ajira, dhamana polisi, mahakamani, hati za kusafiria n.k na ikawa ngumu kumpata mtendaji wakati wenyeviti mara zote husainia watu na kuwagongea mihuri baaa ya kuwafuata majumbani kwao ambapo panaeleweka na wananchi wote waliomchagua.

KIMSINGI 
Kama kuna ulazima wa kuwanyang'anya mihuri wenyeviti wa mitaa, basi;

1. Suala hilo litazamwe kwa mtazamo mpana ili lisilete migogoro isiyo na sababu kwan wenyeviti ni nguzo muhimu katika maendeleo ya jamii wanamoishi.

2. Kwa kuwa wenyeviti wa mitaa ni sehemu muhimu katika utawala wa halmashauri husika (ngazi ya kata), basi ni jukumu la halmashauri kuwapatia semina elekezi za utawala bora na majukumu yao katika nafasi wanazohudumu kwan wengi wao hupata ujuzi na maarifa katika kuhudumu nafasi zao (mazoea) ukizingatia huchaguliwa na wananchi pasipo kupeleka cv zao mahala popote kwa mchujo.

3. Pia wenyeviti wana wajibu wa kujifunza miongozo na mipaka ya kazi zao ili wasitende yaliyo juu yao (ultra vires)

3. Kama wenyeviti wa mitaa wana mihuri ambayo wanaitumia kwa mujibu wa sheria, basi ni lazima itungwe sheria nyingine ya kiwanyang'anya hiyo mihuri na sio kwa utaratibu wa kuikusanya kama mafungu ya nyanya sokoni na wanaweza kuikabidhi waliyonayo na kuchonga mingine na kuendelea kuitumia na wasoweze kubanwa na sheria.

Athman Fimbo, Msomaji;
NAOMBA KUWASILISHA.
Soma HAPA Msimamo wa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.