LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA WATAKIWA KUCHANGIA DAMU KWA WINGI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Wananchi mkoani Mwanza  wametakiwa  kujitolea kuchangia damu, ili kuweza kuokoa maisha ya mama mjamzito na mtoto  ambao  wamekuwa  wakipoteza maisha kwa ukosefu wa damu.

Hayo yalisemwa jana na ofisa Uhamasishaji wa Kitengo cha  Damu Salama kanda ya Ziwa Bernadino Medaa, alipokuwa akizungumza na gazeti hili.

Medaa alisema, ili kuweza kuokoa maisha ya mama mjamzito na mtoto, ni vema  wananchi wawe na utaratibu wa kuchangia damu  katika hospitali mbalimbali zilizopo mkoani hapa.

Pia alisema, wanawake wengi ndio wanakabiliwa na uhitaji wa damu hasa  wajawazito wakati na baada ya kujifungua sambanba na watoto , hivyo ni vema kila mwananchi  kujitolea ili kuweza kuokoa maisha ya wahitaji wa huduma hiyo.

Aliongeza kuwa,kila mwananchi  anatakiwa kuchangia damu kwa hiyari,  itakayosaidia kuokoa maisha ya mgonjwa ambaye anahitaji  huduma hiyo.

"Jamii inatakiwa itambue umuhimu wa kutoa damu kwa hiyari ili kuweza kuoko maisha ya mgonjwa, kwani wenzetu wa nchi nyingine  wanajitahidi kuchangia  kwa wingi, ili kuondoa tatizo la ukosefu wa damu kwenye hospitali na kunusulu maisha ya mgonjwa,"alisema Medaa.

Aidha aliiomba serikali kushirikiana na kitengo hicho,kuhamasisha kuelimisha  jamii kuhusu umuhimu wa uchangiaji damu salama kwani mwitikio ni hafifu.

No comments:

Powered by Blogger.