LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA FUPI YA ZOEZI LA KUHARIBU BIDHAA ZISIZOKIDHI VIWANGO VYA UBORA NA USALAMA KANDA YA ZIWA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

TAARIFA FUPI YA ZOEZI LA KUHARIBU BIDHAA ZISIZOKIDHI VIWANGO VYA UBORA NA USALAMA KUTOKA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA – KANDA YA ZIWA TAREHE 01/10/2015.

1.   UTANGULIZI
Mamlaka ya Chakula na Dawa ni Taasisi ya Serikali iliyoundwa Chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali ikiwa na jukumu la kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za chakula, Dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii kwa kusimamia sheria Na 1, ya mwaka 2003, ya Chakula, Dawa na Vipodozi.
 
Ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) katika utekelezaji wa mpango kazi wake wa mwaka wa fedha 2016/17 hadi sasa imeendesha kaguzi mbalimbali za ufuatiliji wa chakula, dawa za binadamu na mifugo na vipodozi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Lengo likiwa ni kufuatilia utekelezaji wa Sheria Na 1 ya mwaka 2003 ya Chakula Dawa na Vipodozi (TFDC Act No 1, 2003) kwa wasindikaji, wauzaji wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.
 
Katika kaguzi hizo hususani uliofanyika katika Manispaa ya Musoma mnamo tarehe 27/8- 02/09/2016 baadhi ya bidhaa zilikamatwa kwa kukiuka matakwa ya sheria na hivyo kuzuiliwa ili ziharibiwe kwa mujibu wa taratibu na mwongozo wa kuharibu bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu ili kulinda afya ya jamii.
 
Katika ukaguzi huo,vipodozi mbalimbali vyenye uzito wa Kg 40 (tani 0.4) na thamani ya TZS 615,000 ambavyo havina usajili wa Mamlaka pamoja na vipodozi vilivyopigwa marufuku (vyenye viambato vyenye sumu) vilikamatwa.
 
Aidha dawa mbalimbali zenye uzito wa Kg 18 (tani 0.18) na thamani ya TZS 3,250,000 ambazo hazina usajili wa Mamlaka ama kutunzwa na kuuzwa katika majengo yasiyoruhusiwa kuuza/kutunzia dawa hizo zilikamatwa katika zoezi la ukaguzi na zimeharibiwa katika zoezi hili.
 
Kwa upande wa Chakula, bidhaa mbalimbali zenye uzito wa Kg 3,1450 (tani 3.145) vyenye thamani ya TZS 3,777,100 vilikamatwa katika soko. Baadhi ya bidhaa hizo ni chumvi aina ya kaysalt yenye maelezo katika kifungashio  FOR SALE IN KENYA ONLY  na mafuta ya kula aina ya UFUTA katika maduka mbalimbali kutokana na kuingizwa nchini bila kuzingatia taratibu za uingizaji bidhaa nchini, kutokuwa na usajili kutoka Mamlaka na pia kukinzana na kanuni ya uwekaji wa lebo kinyume na Sheria sura 219.  Aidha vyakula vingine ambavyo havijasajiliwa na Mamlaka, ama vilivyokwisha muda wa matumizi pamoja na vyenye viwango duni vilikamatwa katika soko.
Kwa ujumla bidhaa zote zilizoharibiwa na ofisi ya Kanda ya Ziwa kwa chakula na vipodozi vina thamani ya TZS 7,642,100 na uzito wa tani 3.725
 
Bidhaa zote hizi zinaharibiwa kutokana na uwezekano wa kuisababishia madhara jamii kutokana na uduni, kutofahamika kwa viwango vya ubora na usalama pamoja na kukinzana na matakwa ya Sheria ya Chakula Dawa na Vipodozi Na. 1 ya mwaka 2003.
 
WITO
Tunawaomba wafanyabiashara ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba kuzingatia matakwa ya sheria ya Chakula Dawa na Vipodozi Na. 1 ya 2003 kwa kuhakikisha kuwa bidhaa wanazozalisha, wanazonunua, wanazouza, wanazotunza na kusambaza ni zile tu zinazokidhi vigezo vya ubora, usalama na ufanisi ili kumlinda mtumiaji wa bidhaa hizi.

No comments:

Powered by Blogger.