LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAN TRADE YAWAHIMIZA WAJASIRIAMALI WA ASALI NCHINI KUFUATA KANUNI ZA UBORA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Wajasiriamali wa bidhaa ya  asali nchini wameombwa kutumia vifungashio vyenye ubora, ili kuendana na kanuni za ubora sambamba na kuhamasisha wateja, kwani soko la ndani na nje la bidhaa hiyo lipo.

Wito huo umetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TAN TRADE) Edwin Rutageruka wakati akizungumza na gazeti hili  kwa njia ya simu.

Rutageruka alisema, wadau wa bidhaa ya asali wengi  wao, hawatumii vifungashio vilivyo bora na vinavyokubalika na  kuendana na kanuni za ubora, badala yake wanatumia chupa za mvinyo wa konyagi ambazo ni hatari kwa afya ya walaji.

" Wauzaji wa asali nchini wengi wao wanatumia chupa za mvinyo wa konyagi,jambo ambalo alikubaliki kiafya na aliendani na kanuni za ubora, hivyo nawaomba watumie vifungashio vilivyo bora na kuendana na soko la ndani na nje," alisema Rutageruka.

Pia alisema, wanampango wa kupiga marufuku kutumia vifungashio vya mvinyo wa chupa za konyagi ili kuboresha bidhaa hiyo itakayopelekea kupanuka kwa soko.

Hata hivyo aliwaomba wananchi kutumia bidhaa hiyo katika matumizi ya kila siku kwani ni nzuri kwa afya.

Aidha alisema, ili kuendeleza sekta ya asali nchini  mamlaka hiyo ikishirikiana na Sido na Tbs mwezi semptemba mwaka huu waliandaa mafunzo mkoani Singida yaliyowashirikisha wadau wa asali kutoka wilaya zote za mkoa huo.

Vilevile alisema, kupitia mafunzo hayo washiriki hao walipata fursa ya Kuelekezwa namna ya kuchakata na kujua ubora wa  asali, inapotoka, jinsi ya kufungasha kwa kutumia vifungashio bora na masoko yanavyo patikana.

Kadhalika alisema, wanatarajia kutoa mafunzo kama hayo mkoani Tabora ifikapo mwezi Desemba mwaka huu,ili kuendeleza sekta hiyo sambamba na kuwajengea uwezo wajasiriamali ili waweze kuingia katika soko la ushindani ndani na nje ya nchi.

No comments:

Powered by Blogger.