LIVE STREAM ADS

Header Ads

SIKU YA WATOTO NJITI DUNIANI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying IMG_20161117_120317.jpgNa James Salvatory, BMG Dar
Jana ilikuwa siku ya watoto njiti duniani ambapo hospitali ya Taifa Muhimbili, imeitaka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto kuboresha kitengo cha kutunza watoto njiti ikiwemo huduma ya kangaroo ambayo ni muhimu kwa kupunguza vifo vya watoto wachanga.

Kaimu Mkurugenzi wa huduma za upasuaji, Julieth Magandi, alisema kuwa wito huu unatokana na kusahaulika  kwa watoto wanaozaliwa njiti na kuwataka watoa huduma kujitolea kwa wito na kikamilifu ili kuokoa maisha ya watoto hao.

Aidha Magandi aliwaagiza wafanyakazi wote  wa Muhimbili wanaohusika kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ili kuokoa maisha ya watoto.

"Tunatoa wito kwa watoa huduma wenzetu kuwa shughuli hii ifanyike kwa ukamilifu, kujitolea bila kujali muda ili tuweze kupunguza upototeaji wa maisha ya watoto hawa," alisema magandi.

Kwa upande wake bigwa wa magonjwa ya watoto wachanga  Dkt.Augustine Masawe amewasihi akinamama wajawazito kuwa makini  ikiwa ni pamoja na kuwa na afya nzuri wakati wa ujauzito na kufuata ushauri wa daktali.

"Inatakiwa wakina mama wajawazito kuwa na afya nzuri na kama mama ana tatizo ni vema kuwahi keen vituo vya afya mapema kama anatatizo aweze kutibiwa mapema ili kuepusha tatizo hilo," alisema masawe.

No comments:

Powered by Blogger.