LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAFULILA ATIMKA NCCR MAGEUZI. WADAU WATOA MAONI YAO.

Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, (NCCR-Mageuzi) David Kafulila, amekihama chama hicho huku akieleza kuwa anajiandaa kuhamia Chadema.

Kafulila amethibitisha taarifa hizo na kusema tayari ameshawasilisha barua ya kujivua uanachama wa NCCR na kujiunga Chadema leo.

#Maoni
Nani atakayedumu kwenye chama chake?
NA KIBONA DICKSON

Dunia inabadilika,Siasa zinabadilika,Vyama vinabadilika na kufa,watu wanabadilika na wanasiasa wanabadilika pia.Kwa hiyo hakuna mwanachama wa kudumu wa chama cha siasa.

Ni kujidanganya, mtu anapodai kuwa anaweza kuwa mwanachama wa kudumu wa ccm au chadema au Nccr au TLP au chama chochote.

Baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa Tarime,hayati Chacha Wangwe,kilichotokea mwaka 2008,Charles Mwera aliteuliwa kugombea ubunge na kushinda kwa tiketi cha  Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA.

Mwaka 2010, wakati mchakato wa kura za maoni ndani ya chama kwa ajili ya kumpata mgombea,Mwera aliangushwa na Mwita Mwikabe Waitara.Waitara alihamia CHADEMA kutoka CCM baada ya kushindwa kura za maoni  kwa ajili ya uchaguzi mdogo mwaka 2008.

Baada ya kuangushwa kwenye kura za maoni,Mwera alihamia chama cha wananchi-CUF na kukabidhiwa zawadi ya kugombea ubunge Jimbo lilelile la Tarime.

Oktoba 2010,Fatma Maghimbi aliyewahi  kuongoza kambi ya upinzani bungeni,alijiondoa rasmi CUF na kujiunga na CCM.Ilielezwa,uamuzi wake ulitokana na  kukosa kuteuliwa tena kuwa mbunge wa viti maalum.

Mwaka 2010,John Magale Shibuda aliposhindwa kwenye kura za maoni ndani ya ccm,aliamua kuhamia CHADEMA ili apewe nafasi ya kugombea ubunge.

Aliposhinda na kuwa mbunge,maisha yake yalikuwa ya kusuguana na chama chake.Uchaguzi mkuu wa  2015 aligombea kupitia  chama cha TADEA.

John Guninita, aliwahi kuwa mwenyekiti wa CCM  wa mkoa wa Dar e S salaam.Anasifika kwa kutangatanga kwenye vyama vya siasa kwa kile kinachoelezwa  kuwa ni  “malengo yake binafsi ya kusaka madaraka”

Baada ya uchaguzi mkuu wa 1995,Guninita,aliondoka CCM na kuhamia CHADEMA. Baadaye,alirejea CCM na kufanikiwa kuwa mwenyekiti mkoa wa Dare es Salaam.Mwaka 2015,alijiunga tena upinzani kutoka na kile kilichoitwa upepo wa Lowassa.

Steven Wassira,ni  mwanasiasa  aliyefanikiwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi  ndani ya  CCM na serikali zake,hasa awamu ya nne.Kabla ya kurejea CCM,alikuwa mwanachama wa NCCR-Mageuzi na aliwahi kuwa mbunge kupitia chama hicho.

Baada ya kupoteza ubunge,Wasira aliamua kurejea CCM kwenda kusaka madaraka.Aligombea na ubunge na kushinda katika  jimbo la Bunda,akateuliwa kushika nafasi za  uwaziri katika serikali ya rais mustaafu Jakaya  Kikwete.

Laevicia Ghat Musore aliondoka   Chadema na kujiunga na NCCR-mageuzi novemba 2010.Mwisho wa uanachama wake Chadema ulitokana na kutoteuliwa kuwa  mbunge wa viti Maalumu.

Anna Senkoro katika uchaguzi mkuu wa 2005,aliandika historia mpya tanzania  kwa kuwa mwanamke wa kwanza kugombea urais kupitia chama cha PPT- Maendeleo.Baada ya kushindwa kupata madaraka ya urais,mwaka 2007,Anna aliamua kujisalimisha  CCM
James Millya,alihamia CHADEMA akitokea CCM ambako alikuwa kiongozi ndani ya Umoja wa vijana wa CCM(UVCCM).

Mwaka  2010,David Kafulila aliondoka CHADEMA kwenda NCCR-mageuzi na kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la Kigoma kusini,alishinda.

Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 Samweli Sitta na Harryson  Mwakyembe,wanaelezwa kuanzisha chama kipya-chama cha kijamii(CCJ) wakiwa ndani ya CCM.Walimtanguliza Fred Mpendazoe ahamie  CCJ ili  kuwatengenezea njia.

Fred Mpendazoe aliondoka CCM ili kujiunga na CCJ,hivyo alipoteza sifa ya kuendelea kuwa  ubunge wa Kishapu.Alipotambua,maswahiba zake,Sitta na Mwakyembe wamemtosa, alijiunga na CHADEMA.

Sambwe shitambala,aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya  aliwahi ondoka CCM na kujiunga CHADEMA,kisha akatoka CHADEMA na kurejea kwao CCM.

Wilfred Lwakare alikuwa  mbunge wa Bukoba mjini kupitia chama cha wa CUF na kuongoza kambi ya upinzani (2000-2005).Kuelekea uchaguzi wa 2010, alikihama chama cha CUF na kujiunga na  CHADEMA.Uchaguzi wa 2015,aligombea na kushinda ubunge Bukoba mjini kupitia Chadema.

Mabere Marando anayesifika kwa kupigania mageuzi nchini,ni muasisi wa chama cha Nccr Mageuzi.Mwaka 2010 alikihama chama alichokiasisi mwenyewe na kujiunga na chadema.Nccr Mageuzi inaelezwa kufia mikononi mwa mwanyekiti wa sasa,James Mbatia ambaye pia ni mbunge wa Vunjo.

Zitto Kabwe,ni Mwanasiasa mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kustahimili misukosuko.Zitto anaelezwa kujenga  na kuipigania Chadema tangu ujana wake.Akiwa katika kwenye mtafaruku na viongozi wake,alisema “ atakuwa wa mwisho kuondoka Chadema” lakini mwaka 2014 alijiunga na chama cha ACT wazalendo.

Dk Wilbroad Slaa,aliyekuwa katibu mkuu wa chadema,amekijenga chama hicho kwa moyo kujitoa,uwezo wake mkubwa wa kiuongozi na kisiasa na maumivu ya mwili kutoka 1995-2015.

Lakini tarehe 1 septemba 2015 aliitangazia dunia kuwa anaachana na siasa za vyama vingi kutokana na kile alichosema kukaribishwa chamani watuhumiwa wakuu wa ufisadi.

Funga kazi ni Waziri mkuu mustaafu,Edward Lowassa,aliyekuwa mgombea urais wa chadema na kuungwa mkono na umoja wa katiba ya wananchi(UKAWA).

Lowassa,amekulia ccm.Amelelewa na ccm.Ametumia nguvu zote za ujana wake kuijenga ccm.Siku zote za ujana wake ameiunga mkono ccm kwa mema na mabaya(kusigina rasimu ya warioba).

Ameshika madaraka ndani ya serikali kwa muda mrefu.Ameimba kila wimbo unaofaa kuimba ili kuisifia ccm.Wimbo wa mwisho kuimba ulikuwa “ hakuna chama kama ccm kwa sera nzuri”

Julai 28,2015,katika umri wa uzee wake,Lowassa aliitangazia watanzania na dunia kwa kusema “ ccm si baba yangu wala mama yangu.”  Siku hiyo,Lowassa na mkewe Regina Lowassa, walikabidhiwa rasmi kadi za uanachama wa chadema.

Baada ya siku kadhaa,aliyekuwa hasimu wake ndani ya ccm,Waziri mkuu mustaafu,Fredrick Sumaye aliondoka CCM na kuhamia vyama vya upinzani.Wote wawili,Lowassa na Sumaye ni wajumbe wa kamati kuu ya Chadema.

Hakuna mwanachama wa kudumu wa chama cha siasa.Wanachama waliopo wa vyama vya siasa ni wanachama watarajiwa wa vyama vingine.
kibonadickson@ymail.com

No comments:

Powered by Blogger.