LIVE STREAM ADS

Header Ads

OFISI YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM YAUNDA KIKOSI CHA WANASHERIA 35 KUTATUA KERO ZA WANANCHI BURE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na James Salvatory BMG Dar
Katika kuhakikisha kero za wananchi zinatatuliwa ikiwemo migogoro ya ardhi katika Jiji la Dar es salaam, Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa huo imeandaa mkakati wa vijana wanasheria 35 ambao watatoa huduma ya msaada wa sheria bure kwenye wilaya zake.

Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda, amesema uteuzi huo wa wanasheria unaenda sambamba na utatuzi wa kero mbalimbali katika manispaa zilizopo katika Jiji hilo kwa kushirikiana na wakuu wa wilaya.

Aidha Makonda amesema lengo la kuwateua wanasheria hao ni kuhakikisha migogoro ya ardhi pamoja na mirathi inatoweka kabisa na kukoma katika Jiji hilo na kuwaomba wanasheria hao kuzingatia maadili wakati wa utekelezaji wa majuku yao na kuepukana na vitendo vya rushwa.

Makonda ameongeza kuwa wananchi wengi wamekuwa wakilalamika juu ya ucheleweshaji wa kesi hasa katika ardhi na kuwataka wanasheria hao wawe mwarobaini changamoto hizo.
Katika hatua nyingine, Makonda amempatia kiasi cha shilingi laki mbili na kutoa ahadi ya million moja kwa kila mwezi, kwa kijana Andrew Komba ambaye ametelekezewa mtoto na mke wake  mara baada ya mototo huyo kuwa na matatizo ya uvimbe hali iliyompelekea mototo huyo kushindwa kutembea na hata kukaa kutokana na maradhi yanayomsibu.
Naye Mkuu wa Wilaya wa Temeke, Felix Lyaniva, amesema uteuzi wa wanasheria hao umekuja wakati muafaka kufuatia kauli ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli, la kuwatetea  wanyonge na kuwaasa kuwa changamoto kubwa kwa wananchi ni juu ya uelewa washeria hali inayochangia ucheleweshaji
wa kesi  Mahakamani .

No comments:

Powered by Blogger.