LIVE STREAM ADS

Header Ads

KUMEKUCHA BAVICHA KANDA YA ZIWA VICTORIA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Baadhi ya viongozi wa mabaraza ya Chadema wilayani Nyamagana wakimsikiliza Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa Victoria, Meshack Micus (kulia), wakati akizungumza kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
#BMGHabari
Diwani wa Kaya ya Butimba, John Pambalu, akizungumza juzi kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kimewapa semina maalumu viongozi wa baraza la Vijana wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza ili kuendelea kuimarisha uhai wa chama hicho.

Katibu wa chama hicho Kanda ya Ziwa Victoria, Meshack Michael, amesema baada ya semina hiyo kukamilika mkoani Mwanza pia yatawafikia viongozi wa mikoa ya Geita na Kagera ambayo inajumuishwa ndani ya kanda hiyo.

"Tunaenda kutengeneza Chadema ambayo ni nzuri zaidi na yenye kueleweka kwa wananchi huku tukizingatia misingi ya chama ikiwemo kuwania uongozi kuanzia ngazi ya chini ili kukijenga chama kwa misingi ya katiba". Wamedokeza baadhi ya viongozi wa Bavicha Wilani Nyamagana.

Katika semina hiyo, diwani wa Kata ya Butimba, John Pambalu, amewapongeza viongozi wa Bavicha wilani Nyamagana kwa kudumisha umoja na mshikamano na hivyo kuhimiza umoja huo kuwa endelevu ili kuiimarisha zaidi chadema.
Sikiliza sauti HAPA Au play hapo chini
 Tazama picha zaidi HAPA

No comments:

Powered by Blogger.