LIVE STREAM ADS

Header Ads

SAKATA LA KUHAMISHA MACHINGA JIJINI MWANZA.

Kama ulikuwa hujui kwamba mgambo ni jeshi la akiba, Machinga weka bidhaa zako katikati ya Mitaa ya Jiji la Mwanza ikiwemo Makoroboi ndo utajua.

Kumbuka hadi sasa zoezi la kuwaondoa Machinga katikati ya mji (Jijini Mwanza) linaendelea vyema. Ukiona mtu analia jua ni jiwe tu la gizani kwani lengo ni zuri, kuupanga vyema mji wa Mwanza.
Zoezi lilianza jana japo lililalamikiwa na baadhi ya machinga kwamba wanapelekwa maeneo yasiyo rafiki kufanyia biashara ikiwemo Kiloleli

Pia kuliibuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanahabari wakiwalalamikia polisi kuingilia utendaji kazi wao. Baadhi ya Polisi walikuwa wakiwashinikiza kutowahoji machinga badala yake wawaji kiongozi kama wakuu wa Wilaya za Ilemela na Nyamagana. Si vyema mihimili hii kuingiliana kwenye majukumu. Baadhi ya polisi wenye hiyo tabia waache mara moja.

No comments:

Powered by Blogger.