LIVE STREAM ADS

Header Ads

SIKU YA UKIMWI DUNIANI, ULIPOANZIA UGONJWA HUO PATUMIKA KUELIMISHA WANANCHI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Na Mac Ngaiza, Sauti ya Mnyonge
Katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani 2016, serikali ya mkoa wa Kagera imetumia siku hiyo kutoa elimu juu ya maambukizi ya UKIMWI, upimaji na utumiaji wa dawa za kurefusha maisha, katika kata ya Kanyigo halmashauri ya Misenyi, ambapo ugonjwa wa UKIMWI ulianzia mwaka 1983.

Mratibu wa UKIMWI mkoani humo Dr. Abeid Mbelengo, amesema kuwa Kagera iko chini kwa maambukizo ikilinganishwa na mikoa mingine, kwa kuwa na asilimia 4.8 kitaifa, ingawa kiprogram mkoa upo katika asilimia 2.5 ya maambukizi, kutoka 7.8 ya maambukizi mwaka 2013.


Huwepo wa visiwa, na ujirani na nchi nyingine umetajwa katika makala hii kusababisha kuendelea kuwa kikwazo cha uwepo wa maambukizo.

Changamoto kuu katika kupambana na maambukizo ya virusi vya UKIMWI, ni namna ya kuhakikisha elimu inayotolewa inatumika ipasavyo kwa wanaoishi na wasiyo na virusi hivyo, ingawa mafanikio ya kuzuia maambukizo ya kutoka kwa mama kwenda kwa watoto yameanza kuonekana, ingawa ni lazima upimaji upewe kipaumbele kwanza.

Takwimu za UNAIDS zinaonesha watu milioni moja na laki nne wanaishi na virusi vya UKIMWI, ilhali Afrika Kusini ikiwa na watu zaidi ya milioni 10 wanaoishi na virusi hivyo.
tanzania-2015

No comments:

Powered by Blogger.