LIVE STREAM ADS

Header Ads

VINARA WA MASHAIRI KWENYE SHINDANO LA MASHAIRI LA MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAPATIKANA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
 Na James Salvatory, BMG Dar
Hatimaye Mwanamashairi, Dotto Rangi Moto (mwenye bahasha), ameibuka mshindi wa kwanza katika tuzo ya ushairi iliyoandaliwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita, ambapo utunzi wake wa shairi lijulikanalo kama Mwanangu rudi nyumbani umeweza kumpatia ushindi huo.

Shindano hilo lilikuwa la aina yake, lilifanyika jana katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam ambapo jumla ya washiriki 40 waliweza kushiriki kwenye tuzo hizo na hatimaye kuibuka kumi bora na kubaki tatu bora na kuweza kujinyakulia zawadi zao.
 Mshindi wa pili katika tuzo hizo ni Omary Bakari aliyetunga shairi lenye kichwa cha Kichapwi, Wimbi kuu na kufatiwa na Nasoro Mohamed aliyeshika nafasi ya tatu.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza amekabidhiwa kiasi cha fedha taslimu shilingi laki lano, mshindi wa pili laki tatu na mshindi wa tatu laki mbili.

Zawadi hizo  zimekwenda sambamba na washindi wa nafasi ya nne hadi 10 ambapo kila mmoja amepatiwa  zawadi ya shilingi laki moja ikiwa ni motisha ili waweze kufanya vizuri katika shindano lijalo.
Mmoja wa washiriki aliyeweza kuingia kumi bora, Sikudhani Jalala amwasihi wenzake kutokata tamaa na matokeo waliyopata na kuwataka wajipange umpya katika shindano lingine litakalo la msimu wa tatu.
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi

No comments:

Powered by Blogger.