LIVE STREAM ADS

Header Ads

DIWANI WA KATA YA NKENDE WILAYANI TARIME AWAKATIA BIMA ZA AFYA WANANCHI WAKE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Diwani wa Kata ya Nkende wilaya ya Tarime mkoani Mara (CCM), Daniel Komote, akizungumza juzi wakati wa kukabidhi kadi za Bima ya Afya za CHF kwa kaya 100 katika kata hiyo alizozisadia ili kupata huduma bora za afya. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga.
Na MaraOline
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime(DMO) Dr Calvin Mwasha akielezea wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF)
 Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Glorious Luoga akamkibidhi kadi ya CHF mmoja wa wakazi wa kata ya Nkende
 Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Glorious Luoga akamkibidhi kadi ya CHF mmoja wa wakazi wa kata ya Nkende.
Diwani wa CCM awakatia wananchi wake bima ya afya, kaya 100 zenye watu 600 zanufaika.

Diwani wa Kata ya Nkende Daniel Komote(CCM) ameziwezesha kaya 100 kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) ambapo watu 600 kutoka kaya hizo ambazo watanufaika na msaada huo.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga amekabidhi kadi za CHF kwa  familia zilizonufakika na msada huo leo asubuhi na kuagiza wananchi  wote wenye kadi za bima ya afya ya jamii kuwa wanapata huduma ya matibabu bila usumbufu wowote.

Kwa upande wake Komote amesema ameamua kutoa msaada huo ili kuwezesha kaya hizo ambazo zina kipato cha chini wakiwemo wazee na walemavu kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu.

Komote ameweka historia ya kuwa diwani wa kwanza kuwezesha wananchi wahitaji kujiunga na Bima ya Afya ya Jamii katika Hamlshauri ya Mji wa Tarime

No comments:

Powered by Blogger.