LIVE STREAM ADS

Header Ads

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO AHUDHURIA MCHEZO WA KUMUENZI MCHEZAJI WA MBAO FC ALIYEFARIKI UWANJANI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, jana akizungumza kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, Mhe.Nape Nnauye, kwenye mchezo wa hisani kati ya timu za UMISETA wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza, uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Mhe.Wambura, alisema Serikali haijayafuta mashindano ya UMITASHUMITA na UMISETA na kwamba imejipanga vyema ili kuiendeleza michezo hiyo mwaka huu 2017 kwa kuondoa dosari zote zilizojitokeza hapo awali na kusababisha kuahirishwa mwaka jana.

Lengo la mchezo huo ilikuwa ni kumuenzi aliyekuwa mchezaji wa timu ya soka ya vijana chini ya miaka 20 ya Mbao Fc inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Isamail Khalifan Mrisho ambaye Disemba 04 mwaka jana, alifariki dunia akiwa uwanjani kwenye mchezo baina ya na timu yake na Kagera Sugar huku kiingilio kilichopatikana kwenye mchezo huo kikiwasilishwa kwa familia ya mchezaji huyo.

Mchezo huo uliandaliwa na taasisi ya soka nchini iliyomlea mchezaji huyo ya The Football House kwa ushirikiano wa karibu na taasisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Mama Angelina Mabula iitwayo Angeline Foundation.

Hadi dakika 90 zinatamatika, timu ya kombaini ya Nyamagana iliibuka mshindi kwa ushindi wa mabo2-1. Mabao ya Nyamagana yalifungwa na Rajesh Kotecha na Kuzaifa Mdabiru huku Ilemela wakipata bao la kufutia machozi baada ya mchezaji wa Nyamagana Jefta John kujifunga.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, alisema Serikali haijayafuta mashindano ya UMITASHUMITA na UMISETA hivyo imejipanga vyema mwaka huu ili kuendeleza michezo hiyo mwaka huu kwa kuondoa dosari zilizojitokeza hapo awali na kusababisha mwaka jana kuahirishwa.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonald Masele, alisema wilaya yake imejipanga kuhakikisha inaendeleza mchezo wa soka ambapo imeanzisha timu kwa kila soko la machinga wilayani humo hatua ambayo itasaidia kuukuza mchezo huo.
Mkurugenzi wa taasisi ya The Football House, Mbaki Mutahaba, alisema taasisi hiyo itaendelea kumuenzi mchezaji wake Ismail Khalifan Mrisho huku akiwasisitiza vijana kutumia vyema vipaji walivyonavyo kama ilivyokuwa kwa Mrisho ambaye ameacha alama ya soka nyuma yake baada ya umauti kumkuta.
Kaka wa marehemu Ismail Khalifan Mrisho, aitwaye Athman Kitwana, akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya familia kwa namna ambavyo wadau mbalimbali walivyojitoa kumwendeleza kipaji chake, kusaidia kwenye msiba wake na namna wanavyoendelea kumuenzi baada ya umauti.
Wazazi wa marehemu Ismail Khalifan Mrisho, kushoto ni  Rehema Mfaume (mama) na kulia ni Khalifan Mrisho (baba)
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, pamoja na viongozi wengine wakimkumbuka marehemu Ismail Khalifan Mrisho.
Wanaamilia wakimkumbuka marehemu Ismail Khalifan Mrisho.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, akisalimiana na wasimamizi wa mchezo huo
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, akisalimiana na wachezaji wa Kombaini Nyamagana
Viongozi wa taasisi ya The Football House wakisalimiana na wachezaji
Kombaini UMISETA Ilemela (jezi nyeupe), wakisalimiana na Kombaini UMISETA Nyamagana
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa mchezo baina ya Kombaini Nyamagana na Ilemela
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa mchezo baina ya Kombaini Nyamagana na Ilemela
Mpambano baina ya Kombaini Ilemela na Nyamagana ultamatika kwa Nyamagana kuibuka na ushindi wa bao 2-1
Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari Nyamagana na Ilemela wakifuatilia mchezo baina ya Kombaini Ilemela na Nyamagana
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, akizungumza kabla ya mchezo huo.
Afisa Michezo Jijini Mwanza, Mohamed Bitegeko, akizungumzia mchezo huo
Afisa Michezo Manispaa ya Ilemela, Bahati Sosho Kizito, akizungumzia mchezo huo
Baadhi ya viongozi wa taasisi ya The Football House, wakiwa na wadu wengine kwenye mchezo huo baina ya Kombaini Ilemela na Nyamagana uliomalizika kwa Nyamagana kuibuka na bao 2-1 kwenye dimba la CCM Kirumba.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG

No comments:

Powered by Blogger.