LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA DCP: AHMED MSANGI ANATOA TAHADHARI KWA WANANCHI WOTE WA MWANZA NA MAENEO JIRANI KUJIHADHARI/KUJIEPUSHA NA WATU/VIKUNDI VYA WATU AMBAO NI WAHALIFU WALIOKUSUDIA KUJIPATIA FEDHA NYINGI TOKA KWA WANANCHI KWA KUWADANGANYA/ KUWARUBUNI WAJIUNGE NA BIASHARA YA UPATU AMBAPO WANANCHI HAO HUSHAWISHIWA KUWEKEZA FEDHA KIDOGO KWA MUDA MFUPI KATIKA VIKUNDI HIVYO NA BAADA YA HAPO WANAAHIDIWA KULIPWA FEDHA NYINGI ZAIDI YA ZILE WALIZO WEKEZA BILA KUFANYA KAZI YEYOTE. BIASHARA HIYO INATAMBULIKA KWA JINA LISILO RASMI LA KUPANDA MBEGU NA KUVUNA.

HIVI KARIBUNI KUMEJITOKEZA WIMBI KUBWA LA VIKUNDI VYA NAMNA HIYO HAPA JIJI MWANZA NA TAYARI WANANCHI WENGI WAMEIBIWA FEDHA ZAO. KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA UHALIFU WA AINA HII JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEANZISHA NA LINAENDELEA NA MISAKO MAENEO MBALIBALI YA JIJI NA MKOA WA MWANZA, KWA LENGO LA KUBAINI NA KUWAKAMATA WATU/VIKUNDI VINAVYOFANYA UHALIFU HUO. (UPATU)

AIDHA KAMANDA ANATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU VIKUNDI VIFUATAVYO AMBAVYO UPELELEZI UMEONESHA KUWA VINAJIHUSISHA NA BIASHARA YA UPATU AMBAVYO NI; KIKUNDI KINACHOJULIKANA KWA JINA LA AQ POWER CLUB KINACHOMILIKIWA  NA HAPPY ALOYCE MBUYA MIAKA 35, MCHAGA , MKAZI MTAA WA ILIEMELA ENEO LA MAHAKAMANI, MFANYABIASHARA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI BINAFSI IITWAYO AQ CUMPUTER CO.LTD, UPELELEZI UMEBAINI KWAMBA MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU AKISHIRIKIANA NA WENZAKE SABA (7) WAMEFANIKIWA KUKUSANYA FEDHA ZAIDI YA TSH 100,000,000/= KUTOKA KWA WANANCHI AMBAO WALISHAWISHIWA KUJIUNGA NA KIKUNDI CHAKE, PIA UPELELEZI UMEBAINI KUWA AQ POWER CLUB SIO TAASISI ILIYOSAJILIWA KISHERIA BALI JINA LA BIASHARA LA MTUHUMIWA.

TAYARI MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU NA WENZAKE SABA WAMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA PINDI UKIKAMILIKA JARADA LITAPELEKWA KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA DHIDI YAO, AIDHA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ANATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA KIKUNDI/ KAMPUNI BINAFSI YA BEGA KWA BEGA MICRO FINANCE COMPANY LTD, KWANI WATU WENGI WAMEKUJA KURIPOTI POLISI JUU YA KUTAPELIWA FEDHA ZAO NA KAMPUNI HIYO, TAYARI JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEWATIA MBARONI WAKURUGENZI NA BAADHI YA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI HIYO NA MAJALADA YA KESI HIZO YAPO KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA  KISHERIA.
AIDHA JESHI LA POLISI LINAENDELEA KUZIFANYIA KAZI TAARIFA ZA KIINTELEJENSIA KUHUSU TAASISI ITAMBULIKAYO KWA JINA LA AMKA MWANAMKE (AMWA), KWAMBA PIA INAJIHUSISHA NA BIASHARA YA UPATU, UCHUNGUZI UNAFANYWA ILI KUWEZA KUBAINI UKWELI WA TAARIFA HIZO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANAWATAHADHARISHA WANANCHI WOTE WA MWANZA NA MAENEO JIRANI KUJIEPUSHA NA VIKUNDI VYA AINA HII, PIA ANAWAAASA WANANCHI KUJITAFUTIA KIPATO CHA HALALI KWA KUFANYA KAZI HALALI NA SIO KUWEKEZA FEDHA KIDOGO (KUPANDA) NA KUTARAJIA KUPATA FEDHA NYINGI KWA MUDA MFUPI ( MAVUNO). TAMAA YA KUPATA UTAJIRI WA HARAKAHARAKA UMEWAINGIZA WANANCHI WENGI KWENYE HASARA KUBWA ILIYO TOKANA NA KUIBIWA FEDHA ZAO KWANI HAKUNA KIKUNDI/ MTU ANAYEWEZA KUPEWA FEDHA KWA MUDA MFUPI ALAFU BAADA YA MUDA MFUPI ALIPE FEDHA NYINGI ZAIDI. WANANCHI WATAMBUE KUWA HUU NI MTEGO WA WAHALIFU WA KUWAFANYA WANANCHI WASHAWISHIKE KUJIUNGA NA VIKUNDI HIVYO ILI WAWAIBIE.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments:

Powered by Blogger.