LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MWANANCHI TARIME AONYESHA MFANO BORA KATIKA JAMII.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mwandishi wa habari kampuni ya Mwananchi Communication, Waitara Meng'anyi (kulia) akikabidhi begi kwa diwani wa Kata ya Sirari wilayani Tarime, Nyangoko Paul ili akamkabidhi binti ambaye mwandishi huyo amejitoa kumsaidia vifaa vya shule ambapo ametoa begi moja na shilingi elfu 30,000 kwa ajili ya kushona sare za shule.
Na Cleo Newz
Binti huyo akikabidhiwa fedha shilingi (30,000 kwa ajili ya manunuzi ya sare ya shule  kwani binti huyo amedai  kuwa tangu apelekwe kidato cha kwanza mpaka sasa wazazi wake wamekataa kununua sare hizo.

Akikabidhi vifaa hivyo wiki iliyopita, mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communication, Waitara Meng’anyi, alisema meamua kufanya hivyo baada ya kwenda kufanya mahojiano na binti huyo na kubaini kuwa wazazi wake wameshindwa kununua vifaa vya shule ili  kuendelea na masomo huku wakilazimisha binti huyo kukeketwa  na kuguswa na jambo hilo hivyo amejitolea kutoa msaada huo.

“Sisi waandishi wa habari siyo kwamba jukumu letu ni kuandika habari tu wakati mwingine tunapaswa kusaidia jamii  inayotuzunguka ili iweze kutimiza ndoto zake nimeamua kusaidia binti huyu baada ya kunisimulia kisa chake na kuguswa” alisema Waitara.

Aidha mwandishi huyo ametoa msaada wa begi moja na shilingi 30,000 kwa ajili ya kushona sare za shule na kununua mahitaji mhimu ya shule.

Akikabidhi kwa niaba ya Mwandishi huyo Diwani wa kata ya Sirari Paul Nyangoko, alizidi kuwaasa wazazi na walezi kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Binti Huyo ambaye hakutaka jina lake kutajwa mwanafunzi wa kitado cha pili shule ya sekondari Sirari alisema kuwa tangu apelekwe kidato ch kwanza mzazi maybe ni baba wake wa kambo hajawai kununua sare za shule mpaka sasa huku akishikilia madaftari mikononi.

Wazazi wangu hasa mama mazazi amekuwa akinilazimishwa kukeketwa sasa imekataa na nilivyoenda kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kijiji Baba, Mama na kaka walinipiga na kuniumiza sana huku kaka akinitishia maisha naomba serikali inisaidia alisema Binti huyo.

No comments:

Powered by Blogger.