LIVE STREAM ADS

Header Ads

MFANYABIASHARA PETER ZAKARI AINUSURU HOSPITALI YA WILAYA YA TARIME NA ADHA YA MAJI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Mwenyekiti wa kamati ya ukarabati wa hospitali ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Peter Zacharia ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wilayani humo akimiliki pia mabasi ya Zakaria Air Bus, akimimina maji  kwenye ndoo baada ya kutoa msaada wa maji katika hospital hiyo  kwa lengo la kutatua changamoto ya ukosefu wa maji iliyojitokeza kwa takribani wiki moja hospitalini hapo.
Na Cleo Newz
Mganga Mkuu hospitali ya halmashauri ya mji wa Tarime, Calvin Mwasha, akimimina maji kwenye ndoo baada ya kupokea msaada wa gari la maji kutoka kwa Peter zacharia ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ukarabati wa hospitali hiyo na pia mfanyabiashara wilayani humo
Watumishi wa hospitali ya Tarime wakichota maji.

Kutokana na ukame ambao umeashamili maeneo mbalimbali ya nchi na kupelekea baadhi ya vyanzo vya maji kukauka hospitali ya wilaya ya Tarime mkoani Mara kukumbwa na changamoto ya ukosefu wa maji jambo ambalo limemusukuma Mwenyekiti wa Bodi ya ukarabati wa Hospital hiyo Peter Zacharia kutoa Gari kwa ajili ya  kuleta Maji kwa lengo la kutatua changamoto hiyo.

Zacharia ambaye ni mdau wa maendeleo pia Mwenyekiti wa kamati ya ukarabati wa Hospital hiyo  na mfanyabiashara amesema kuwa ameamua kutoa msaada huo wa gari la kusomba maji ili kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika hospital hiyo kwani wagonjwa wamekuwa wakiteseka kwa sababu ya ukosefu wa maji.

“Nikiwa tumboni mwa mama yangu na nilipozaliwa nilijaliwa na mwenyezi Mungu kuwa injinia wa mambo mbalimbali na sasa nausika na magari ya usafirishaji sasa wanachi wa Tarime ninachowalaumu hawataki maendeleo na wanapinga sana mtu ambaye anataka kuwasaidia wanachagua viongozi ambao wanajali posho na maslahi yao tu” alisema Zacharia.

Akipokea Msaada wa maji hayo Matron wa Hospital hiyo Paulina Shirole ametoa shukrani zake na kudai kuwa kipindi cha nyuma takribani wiki moja suala zima la maji limekuwa changmoto kubwa na kupelekea suala zima la usafi kukwama.

Nao baadhi ya wanachi ambao wanauguza katika Hospital hiyo wametoa shukrani zao kutokana na msaada huo huku wakizungumzia hadha waliokuwa wikipata kipindi cha Nyuma kuwa baadhi huduma zimekuiwa zikikwama kwa sababu ya ukkosefu wa maji.

No comments:

Powered by Blogger.