LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAJASIRIAMALI WACHANGIA UKARABATI WA MITARO KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba Steven Shija amepokea mifuko 35 ya saruji yenye thamani ya shs 542,500 kutoka kwa wajasiriamali na mafundi wa eneo la uwanja huo.

Shija alipokea saruji hiyo jana, katika eneo la uwanja huo uliopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza na kuushukuru umoja huo kwa kujitolea  kuchangia ukarabati wa miundomboni ya kupitisha maji taka ambao umekuwa kero kwa mashabiki wanaoenda kushuhudia michezo ya  ligi mbalimbali uwanjani hapo, wanafunzi wa shule ya msingi Kitangiri pamoja na mafundi na wajasiriamali hao.

Pia aliwaahidi kuendelea kuwapa ushirikiano na kuimarisha mahusiano aliyoyaanzisha, maana anaamini hakuna jambo jema na endelevu linaweza kufanywa na yeye binafsi bila kushirikiana na wadau wengine wenye nia njema.

Hata hivyo alisema, mpaka sasa wanajumla ya mifuko 60 ya saruji bado 40 ili kukamilisha mifuko 100 inayohitajika na kuongeza kwamba mbali na saruji zinahitajika fedha za kulipa mafundi, kokoto ndogo tripu tatu, mawe tripu 30, nondo 30,inayogharimu  sh 4.2 milioni.

Vilevile aliwaomba  wadau mbalimbali kuendelea kusaidia kuchangia juhudi hizo, ili kukamilisha ukarabati huo na kuondoa kero hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi wa Uwanja wa CCM Kirumba, Michael Omollo ameahidi kupitia umoja wao wataendelea kusaidia  ukarabati wa miundombinu hiyo, ili kutoathiri shughuli zao.
Isikupite habari hii

No comments:

Powered by Blogger.