LIVE STREAM ADS

Header Ads

MSIMAMO WA WAKALA WA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KUHUSU KEMIKALI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, Dar
Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) wamejipanga kuendelea kuendesha mafunzo kwa wadau wa Kanda ya Mashariki wanaohusika na kemikali ili kuhakikisha kemikali zinatumika vema na kwa njia salama.

Hayo yabebainishwa leo Jijini Dar es salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa wakala hufanya usajili na ukaguzi kwa wadau wote wanaohusika na kemikali wakiwemo waagizaji, watengenezaji, wasafirishaji, watumiaji, wanaosafirisha nje ya nchi au yeyote yule anayehusika na kemikali kwa njia moja au nyingine na ukaguzi huo unahusisha mahali ambapo kemikali zinatumika, zinatunzwa au kuhifadhiwa.

Aidha amesema kuwa kuanzia mwaka 2012 hadi sasa, wadau wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani waliopatiwa mafunzo ni 642 wakiwemo askari wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani Tanzania Bara, wasimamizi wa shughuli za uzalishaji kwenye viwanda, wasambazaji, wasafirishaji wa kemikali pamoja na madereva wanaosafirisha kemikali.,

Amesema hakuna mdau yeyote atakayeruhusiwa kujihusisha na shughuli za kemikali kama hajapitia mafunzo hayo yanayolenga kujua matumizi salama ya kemikali, kuhifadhi, kusafirisha, kutoa bandarini na hata kuagiza kutoka nje ya nchi.

No comments:

Powered by Blogger.