LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


KWAMBA TAREHE 12.01.2017 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASUBUHI KATIKA MTAA WA KABANGAJA KATA YA SANGABUYE JIJI NA MKOA WA MWANZA, SILAHA MOJA ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI AINA YA GOBOLE INAYOTUMIA BARUTI IMEKAMATWA KWENYE CHUMBA NYUMBANI KWA BIGIRE KALEMANI, MIAKA 42, MSUKUMA NA MKAZI WA MTAA WA KABANGAJA, IKIWA IMEFUNGWA KWENYE MFUKO WA SANDARUSI NA KUFUKIWA ARDHINI KISHA JUU KUPANGWA MATOFALI, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERI.

INADAIWA KUWA MAJIRA TAJWA HAPO JUU MWANAMKE MMOJA AITWAYE ASHA BISCO MIAKA 35, ALIKUWA AKIFANYA USAFI CHUMBA CHAKE ALICHOPANGISHA KILICHOPO KWENYE NYUMBA YA MWANAMKE TWAJA HAPO JUU ILI AWEZE KUHAMIA, AIDHA INADAIWA WAKATI AKIENDELEA NA USAFI ALIONA MFUKO WA SANDARUSI CHINI YA ARDHI HIVYO ALIAMUA KUUVUTA TOKA CHINI YA ARDHI AKIJUA NI UCHAFU ILI AKATUPE, NDIPO BAADA YA KUUTOA MFUKO HUO NA KUUANGALIA NDANI ALIONA SILAHA HIYO AINA YA GOBOLE.

AIDHA BAADA YA KUIKUTA SILAHA HIYO MAHALI HAPO BI ASHA BISCO ALIAMUA KUTOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIKWENDA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUIKAMATA SILAHA HIYO. POLISI WANAMSHIKILIA MAMA MWENYE NYUMBA BI BIGIRE KALEMANI KWA MAHOJIANO ZAIDI JUU YA KUPATIKANA KWA SILAHA HIYO AINA YA GOBOLE HAPO NYUMBANI KWAKE,  HUKU UPELELEZI NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO UKIWA BADO UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA KWA KUTOA TAARIFA POLISI MAPEMA ZA WATU AMBAO WANAWAFAHAMU KUWA WANAMILIKI SILAHA KINYUME NA SHERIA ILI WAWEZWE KUKAMATWA MAPEMA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA KABLA SILAHA HIZO HAZIJALETA MADHARA KWA WANANCHI.

KATIKA TUKIO LA PILI
KWAMBA TAREHE 13.02.2017 MAJIRA YA SAA 02:45HRS USIKU KATIKA MTAA WA MAHINA – KANYERERE KATA YA BUTIMBA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA MWANAMUME AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA 25 HADI 30, ALIUAWA KWA KUPIGWA MAWE NA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE HADI KUFARIKI DUNIA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA TUHUMA YA WIZI WA MLANGO WA MBAO MALI YA FILBERT NKWELO, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA MAJIRA TAJWA HAPO JUU MAREHEMU AMBAYE NDIO MWIZI ALIVUNJA DIRISHA LA WAVU LA NYUMBA YA FILBERT NKWELO NA KUINGIA NDANI NA KUIBA MLANGO KISHA WAKATI ANATOKA NJE ILI AONDOKE WATU/WANANCHI WALIMUONA NA KUANZA KUPIGA YOWE YA MWIZI AMBAPO KUNDI KUBWA LA WATU WAKIWA NA MAWE NA FIMBO LILIMVAMIA NA KUMPIGA SEHEMU MBALIMBALI  HADI KUFARIKI DUNIA.

AIDHA HAKUNA MTU YEYOTE ALIYEKAMATWA KUHUSIANA NA KIFO HICHO, ASKARI WANAENDELEA NA UPELELEZI PAMOJA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA MAUAJI HAYO, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFDHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHAMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WAJIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA  YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA LA JINAI, BALI PINDI WANAPOWAKAMATA WAHALIFU WAWAFIKISHE POLISI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAO.

KATIKA TUKIO LA TATU
KWAMBA TAREHE 11.02.2017 MAJIRA YA SAA 18:20HRS JIONI KATIKA ENEO LA NGUDU MJINI BARABARA YA NGUDU “B” WILAYA YA KWIMBA MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA T 183 BKG AINA YA TOYOTA HARRIER LIKIENDESHWA NA MTU ALIYEJULIKANA KWA JINA LA IMAKULATA INYASI @ BYAMUNGU MIAKA 35, MHAYA NA MKAZI WA NGUDU, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO AITWAYE PATRICK YONA MIAKA 04, MSUKUMA MKAZI WA MTAA WA NGUMO B” NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.

INADAIWA KUWA AJALI HIYO IMETOKEA WAKATI MAREHEMU AKIVUKA BARABARA HUKU MWENDESHA GARI AKIWA KWENYE MWENDO KASI, AMBAPO ALISHINDWA KULIMUDU GARI NA KUPELEKEA KUMGONGA MAREHEMU NA KUFARIKI DUNIA. DEREVA WA GARI HILO AMEKAMATWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA KWIMBA KWA AJILI YA UCHUNGUZI.

AIDHA KATIKA TUKIO LINGINE LA TAREHE TAJWA HAPO JUU MAJIRA YA 21:10HRS USIKU KATIKA ENEO LA BUZURUGA KWENYE KISIMA CHA MAFUTA CHA GBP WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA T 211 DFW AINA YA MITSUBISHI FUSO LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA BUSHESHE EMMANUEL @ MISHISHI MIAKA 30, MSUKUMA NA MKAZI WA NYASAKA, LILIMGONGA  MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA BAHATI PETER MIAKA 31,MSUKUMA NA MKAZI WA NYASAKA, AMBAYE ALITELEZA NA KUANGUKA CHINI KISHA KUKANYWAGA KICHWANI  NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO.

INADAIWA KUWA DEVERA WA GARI HILO BWANA BUSHESHE EMMANUEL ALIKUWA ANAPAKIA ABIRI SEHEMU HATARISHI HUKU AKIWA KWENYE MWENDO, HUKU MAREHEMU AKIWA ANAPANDA NDANI YA GARI LAKINI KWA BAHATI MBAYA ALITELEZA NA KUANGUKA CHINI KISHA KUKANYWAGWA KICHWANI NA KUFARIKI DUNIA, DEREVA LA GARI HILO AMEKAMATWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA AFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO AKIWATAKA KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI PINDI WAWAPO BARABARANI, ILI KUEPUSHA VIFO NA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WAPOLISI (M) MWANZA

No comments:

Powered by Blogger.