LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAKUU WA IDARA ZA MAWASILIANO NA TEHAMA KANDA YA ZIWA WATAKIWA KUWEKA TAARIFA MUHIMU ZA SERIKALI KWENYE TOVUTI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mgeni rasmi Katibu Tawala idara ya uchumi na uzalishaji mkoa wa Mwanza, Johansen Bukwali, akifungua mafunzo kwa Wakuu wa Idara za Mawasiliano na Tehama kutoka halmashauri za wilaya na mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhusu Uimarishaji wa Mifumo ya Mawasiliano katika Sekta za Umma. Bukwali amemwakilisha Katibu Tawala mkoani Mwanza, CP.Clodwig Mtweve.
BMG
Wakuu wa idara ya mawasiliano na Tehama kutoka halmashauri za wilaya na mikoa ya Kanda ya Ziwa, wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Tawala idara ya uchumi na uzalishaji mkoa wa Mwanza, Johansen Bukwali, aliyemwakilisha Katibu Tawala mkoani Mwanza.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Tamisemi, Rebeca Kwandu, akizungumza kwenye mafunzo hayo
Mkuu wa Kitengo cha Mifumo wa Mawasiliano PS3 Dar es salaam, akitoa ufafanuzi kuhusiana na mafunzo hayo
Afisa Habari mkoani Mwanza, Atley Kuni, akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya washiriki wengine wa mafunzo hayo
Kutoka kushoto ni Palestirian Masai, Meneja mradi wa PS3 Mwanza, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Tamisemi, Rebeca Kwandu, Mgeni rasmi Katibu Tawala idara ya uchumi na uzalishaji, Johansen Bukwali na Mkuu wa Kitengo cha Mifumo wa Mawasiliano PS3 Dar es salaam
Washiriki wa mafunzo ya Uimarishaji wa Mifumo ya Mawasiliano katika sekta za Umma PS3 wakifuatilia mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo ya Uimarishaji wa Mifumo ya Mawasiliano katika sekta za Umma PS3 kutoka mkoani Mwanza, wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Johansen Bukwali (wa tatu) ambaye amemwakilishi Katibu Tawala mkoani Mwanza
Washiriki wa mafunzo ya Uimarishaji wa Mifumo ya Mawasiliano katika sekta za Umma PS3 kutoka mkoani Kagera, wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Johansen Bukwali (wa tatu) ambaye amemwakilishi Katibu Tawala mkoani Mwanza
Washiriki wa mafunzo ya Uimarishaji wa Mifumo ya Mawasiliano katika sekta za Umma PS3 kutoka mkoani Shinyanga, wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Johansen Bukwali (wa tatu) ambaye amemwakilishi Katibu Tawala mkoani Mwanza
Washiriki wa mafunzo ya Uimarishaji wa Mifumo ya Mawasiliano katika sekta za Umma PS3 kutoka mkoani Mara, wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Johansen Bukwali (wa tatu) ambaye amemwakilishi Katibu Tawala mkoani Mwanza
Timu ya mafunzo ya Uimarishaji wa Mifumo ya Mawasiliano katika sekta za Umma PS3 ikiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Johansen Bukwali (wa tatu) ambaye amemwakilishi Katibu Tawala mkoani Mwanza

Binagi Media Group
Wakuu wa idara za Mawasiliano na Tehama katika halmashauri za wilaya na mikoa ya Kanda ya Ziwa, wametakiwa kuweka taarifa zote muhimu za serikali kwenye tovuti za idara zao ili kuwarahisishia wananchi kupata taarifa hizo kwa wakati.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Tamisemi, Rebeca Kwandu, ametoa agizo hilo hii leo Jijini Mwanza, kwenye mafunzo ya siku nane kwa wakuu hao kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Mawasiliano katika sekta za Umma.

"Tuhakikishe wananchi wanapata huduma inayostahili kwa wakati kupitia mawasiliano na hasa tovuti zetu. Mafunzo haya siyo ya mchezo mchezo hivyo tunategemea baada ya mafunzo haya kila mtu ataweza kutengeneza tovuti mwenyewe na kuweka taarifa zote zinazohitajika".Amesisitiza Kwandu.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano Dar es salaam, Desderi Wengaa, amebainisha kwamba mfumo huo utasaidia serikali kuweka taarifa zake kwa uwazi ikiwemo za utoaji huduma katika sekta mbalimbali tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Tawala mkoani Mwanza, Katibu Tawala idara ya uchumi na uzalishaji, Johansen Bukwali amebainisha kwamba yatasaidia kuimarisha shughuli za utendaji serikalini.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo, Atley Kuni ambaye ni Afisa Habari mkoani Mwanza, amesema mradi wa Uimarishaji Mifumo wa Mawasiliano katika Sekta za Umma, utasaidia kuimarisha upatikanaji wa taarifa sahihi za serikali kupitia tovuti za halmashauri na mikoa nchini.

No comments:

Powered by Blogger.