LIVE STREAM ADS

Header Ads

WACHAPAJI WA NYARAKA ZA SERIKALI WATAKIWA KUJISAJILI SERIKALINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, Dar
Serikali imewataka wafanyabiashara na wachapishaji wa nembo mbalimbali za serikali ikiwemo bendera ya Taifa, kujisajili ili kuwa na kibali cha kufanya biashara hiyo.

Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo, aliyasema hayo jana mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea matumizi sahihi ya nembo za serikali pamoja na wimbo wa Taifa kwa wananchi na viongozi wa kitaifa.

Alisema ni marufuku kwa yeyote kujihusisha na uchapaji na uuzaji wa nembo za serikali bila kusajiliwa ambapo amewataka ambao hawajasajiliwa kufika ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ili kusajiliwa vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha alihimiza matumizi sahihi ya bendera ya Taifa ikiwemo kutumika katika maeneo yanayoruhusiwa kisheria ikiwemo kwenye ofisi za serikali na taasisi za kielimu huku akipiga marufuku matumizi ya bendera za Taifa zilizochakaa.

Alibainisha kwamba kwa viongozi wa kitaifa wanaotumia bendera ya Taifa kwenye magari yao ambao ni Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, bendera hiyo inapaswa kuwekwa upande wa kulia na viongozi wengine wakiwemo spika wa bunge, mawaziri, wabunge, majaji, wakuu wa mikoa na wilaya, bendera hiyo inapaswa kuweka upande wa kushoto.

No comments:

Powered by Blogger.