LIVE STREAM ADS

Header Ads

SALAMU ZA SHUKURANI KUTOKA KWA MDAU GEORGE BINAGI BAADA YA KUPATA MSIBA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

"Nawashukuruni ndugu, jamaa na marafiki kwa namna mlivyojitoa katika mazishi ya rafiki na mama yetu mpendwa Leah Daniel Marwa Binagi aliyefariki dunia Jumapili Januari 29,2017 baada ya kuugua kwa muda.

Mazishi yalifanyika salama nyumbani Kenyamanyori Wilaya ya Tarime mkoani Mara siku ya Jumatano Februari Mosi, 2017. Marehemu Leah Daniel Marwa Binagi alizaliwa mwaka 1963 hivyo hadi umauti unamkuta alikuwa na miaka 64.

Ahsanteni Wanahabari wote ndani na nje ya Tanzania hususani Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mwanza MPC, Umoja wa Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii (Blogs) Tanzania TBN, Taasisi ya OJADACT, Makundi ya Whatsupp kama vile Jambo Tarime, Mwanza Habari, Malunde 1 Blog & Wadau, BMG Tanzania, Binagi Media Group, Kurya Empire, SGI Rock City bila kuwasahau marafiki zangu wote kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na Twitter.

Lakini pia kwa upekee uongozi wa Redio ninayofanyia kazi, 102.5 Lake Fm Mwanza, Alphonce Tonny Kapela kutoka Metro Fm Mwanza na Kijukuu cha Bibi K kutoka Radio Free Africa, Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola, wanafamilia pamoja na wauguzi na madaktari wote waliomuuguza mama.

Sina cha kuwalipa kwa faraja zenu, ila Mungu hatawasahau kamwe kwa Upendo wenu wa dhati. Pia familia ya Binagi kwa ujumla inawashukuruni mno. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina". George Binagi, mwanahabari na mwanzilishi wa mtandao wa habari wa Binagi Media Group ambaye pia ni mmoja wa watoto wa Marehemu Leah Daniel Marwa Binagi.
Ndugu, jamaa, marafiki na wanafamilia wakiwa msibani
Mwinjilisti Davide Binagi (katikati) akitoa akiongoza ibada ya mazishi
Uongozi wa mtaa wa Buguti Rebu, alipokuwa akiishi marehemu ukitoa salamu za pole
Mwenyekiti wa Mtaa wa Chira, alipozikwa marehemu akitoa salamu za pole
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola, akitoa salamu za pole kwa niaba ya waumini wengine
Mwanahabari, Kijukuu Cha Bibi K kutoka Redio Free Afrika akitoa salamu za pole kwa niaba ya wanahabari wengine
Ndugu, jamaa na marafiki wakiaga mwili wa marehemu
Mwili wa marehemu ukipelekwa malaloni
Mwili wa marehemu ukipelekwa malaloni
Mwili wa marehemu ukihifadhiwa malaloni
Mzee Maina Binagi akirusha udongo ishara ya kuuaga mwili wa marehemu. Marehemu alikuwa shemeji yake
Mzee Maina Binagi na mkewe wakiweka shada
Profesa LloydBinagi akiweka shada malaloni. Marehemu alikuwa shemeji yake
Maina Binagi, Kijana wa marehemu akiweka shada
Kijana wa marehemu, Mwalimu Charles Binagi akiweka shada malaloni
Mtoto wa marehemu, George Binagi (kulia) akiweka shada na mchumba wake (katikati) pamoja na shemeji yake (kushoto)
Dada zake na marehemu wakiweka shada
Anjelina Binagi, bintiye marehemu akiweka shada
Mke mwenza na marehemu akiweka shada
Mke mwenza na marehemu akiweka shada
Watoto wa wake wenzie na marehemu wakiweka shada
Zephania Mwita Mang'ache ambaye ni Mtoto wa wifi yake na marehemu akiweka shada
Kushoto ni kaburi la marehemu Leah Daniel Marwa Binagi na kushoto ni kaburi la aliyekuwa mmewe Mzee Daniel Marwa Binagi
Mungu awabariki waendesha bodaboda wilayani Tarime
Mungu awabariki ndugu, jamaa na marafiki

No comments:

Powered by Blogger.