LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA ACACIA YAONYWA KUWAPUNGUZA WAFANYAKAZI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Shaban Njia
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Kassimu Mjaliwa amewataka Wawekezaji wa Kampuni ya Acacia kutowapunguza kazi watumishi wake kutokana na Kauli ya Rais wa Dr, John Magufuli kuzuia usafirishwaji wa Makontena ya mchanga wa dhahabu kwenda nje ya nchi kwa ajili ya uchenjuaji.

Majaliwa aliyasema hayo juzi wakati wa ziara yake ya kushitukiza ya saa moja katika Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Kampuni hiyo ikiwa ni sambamba na uchukua sampo ya mchanga wa dhahabu na kuupeleka kwa mkemia Mkuu wa serikali kwa ajili ya kuupima na kuona kama kuna aina ngapi za madini.

Majaliwa alisema kuwa kwa sasa lazima Migodi iwe wazi kwa Shughuli wanazozifanya ili Watanzania wengi waweze kujua nini kinafanyika na kuondoa fikra potofu baina yao ya kuwa wawekezaji hao wamekuwa wakiiba mali ghafi ya nchi na kupeleka kwao kwa lengo la kujinufaisha huku taifa likibaki bila kitu.

“Watanzania wanataka kujua ni nini kinazalishwa katika Mgodi huo kama ni Dhahabu, Shaba au madini mengine lazima mseme ni kiwango gani cha madini mnachopata hali ambayo itaondoa mining’ono kwa wananchi na mtoe matokeo halisi kwa dhahabu mnayochimba katika Mgodi huo”, Alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Majaliwa pia aliwaagiza wawezaji hao kuhakikisha kuwa wanajenga mitambo ya uchenjuaji wa dhahabu hapa nchini kama sera ya Madini ya Madini ya mwaka 2009 walivyokubalinana Serikali kabla ya kuanza  shughuli zao za uchimbaji wa Madini ya Dhabau hapa nchini.

Pia katika ziara hiyo Waziri Mkuu huyo wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa alipata fursa ya kuangalia makontena zaidi ya 180 yaliokuwepo katika mgodi huo huku akiwaamuru kufungua sili zake ili aweze kuchukua sampo za machanga huo wa dahahabu na kwenda kuupelea kwa Mkemia Mkuu wa serikali ili kuweza kuona ni kiasi gani cha madini yaliopo katika mchanga huo.

Hata hivyo Waaziri Mkuu huyo aliwahakikishia wawekezaji hao kuwa kuwa Serikali ipo pamoja nao na kuongeza kuwa juu ya suala la kusafirisha makontena hayo kwenda nchi za nje kutakuwa na mazungumzo baina ya pande hizo zote mbili na kuongeza kuwa lazima muafaka utapatikana katika siku za baadaye.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Madini kutoka Wakala wa Madini hapa Nchini (TMAA) Eradius Erasto alisema kuwa mapaka kufikia hivi sasa jumla ya Makontena 180 ya mchanga wa dhahabu yapo katika Mgodi huo, 21 yakiwa tayari yapo bandarini wakati 152 yakiwa yapo katika kampuni ya ZAM KAGO ya jijini Dar Es Salaam.

Hata hivyo Erasto alisema kuwa idadi hiyo ya Makontena inaweza kuongezeka kulingana na jinsi ambayo usafirikishwaji umesitishwa hali ambayo inaweza kusababisha mrundikano mkubwa wa makontena hayo katika mgodi huo ambayo bado hayajasafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya uchenjuaji wake.

Nae Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Stewart Hamilton alisema kuwa wao kama Kampuni wanasubiri uamuzi utakaotolewa baina ya mazunguzo ya pande hizo mbili na kuongeza kuwa ni matumiani yake kuwa muafaka utafikiwa na matokeo yatatolewa kwa majibu wa makubalinao hayo.

No comments:

Powered by Blogger.