LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKUBALIANO YA SOKO LA AFRIKA MASHARIKI BADO NI CHANGAMOTO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

James Salvatory, Dar
Imeelezwa kuwa  bado kuna changamoto  katika  makubaliano yaliyowekwa  mwaka 2010 katika nchi za ukanda wa Afrika  Mashariki  hususani kwenye Soko la pamoja la ukanda huo.

Hayo yamesemwa  leo  jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Sera kutoka Taasisi ya sekta binafsi (TPSF)  Gillad Teri kwenye mkutano uliowakutanisha  wanachama wa sekta binafsi na kampuni zinazofanya kazi kwenye soko la  Afrika Mashariki.

Amesema kuwa  kulikuwa na makubaliano  yaliyowekwa 2010 kwa kuruhusu uhuru wa mitaji ,bidhaa na watu kuvuka kwa nchi  za afrika mashariki na  katika hayo makubaliano yalikuwepo, makubaliano madogo 2700 ambayo nchi inapaswa kurekebisha  ni pamoja na  sheria,mifumo na utaratibu kwa lengo la kusaidia kukuza biashara na utengamano kwa nchi za afrika mashariki

 Aidha amesema kuwa   mkutano wa leo una lengo la kuchambua na kutadhimini  kwa yale  makubaliano yaliyowekwa  miaka saba iliyopita kwa  nchi za afrika mashariki kama yanatekelezeka  ili  kuweza kuwasilisha kwa serikali  kwa zile changamoto zinazojitokeza hususani kwenye sheria.

No comments:

Powered by Blogger.