UVUVI HARAMU WAKOMESHWA WILAYANI CHATO MKOANI GEITA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Akizungumza na Maduka online ofisini kwake Bw. Manampa Alisema kuwa ni muda mrefu amekuwa akiwaomba wenyeviti hao kufungua mipaka waliyokuwa wamejiwekea hali ambayo ilipelekea wavuvi haramu kutumia mipaka hiyo kujificha na kukwepa doria ya majini.
"Kiukweli kufunguliwa kwa mipaka ambayo wavuvi haramu walikuwa wakitumia mwanya huo kujificha imesaidia sana kwani kwasasa tumedhibiti hali hii ya uvuvi haramu kwa asilimia kubwa"Alisema Manampa.

Mwenyekiti wa watunza mazalio na makulio ya samaki  Bashiri Manampa  kutoka  Mwaro wa Nyamilembe wilayani Chato mkoani Geita amewashukuru wenyeviti wenzake wa miaro ya Buhungu na nyakakarango kwa kufungua mipaka  ili kukomesha uvuvi haramu ndani ya ziwa victoria.
Akizungumza na Maduka online ofisini kwake Bw. Manampa Alisema kuwa ni muda mrefu amekuwa akiwaomba wenyeviti hao kufungua mipaka waliyokuwa wamejiwekea hali ambayo ilipelekea wavuvi haramu kutumia mipaka hiyo kujificha na kukwepa doria ya majini.
"Kiukweli kufunguliwa kwa mipaka ambayo wavuvi haramu walikuwa wakitumia mwanya huo kujificha imesaidia sana kwani kwasasa tumedhibiti hali hii ya uvuvi haramu kwa asilimia kubwa"Alisema Manampa.
Katika hatua nyingine Bw. Manampa ameongeza kuwa kutokana na ushirikiano huo  watapunguza au kuondoa suala la uvuvi haramu ambalo limekuwa  na changamoto   nyingi  wilayani humo.
Aidha hivi karibuni waziri wa kilimo ,uvuvi na mifugo Dkt Charlse Tizeba alifika wilayani humo na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo ambapo alitoa  onyo kali kwa watu wanao jihusisha na uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na kuongeza adhabu kwa mtu atakae bainika anajihusisha na vitendo hivyo
 Baadhi ya wananchi wa nyamirembe na nyakakarango Bw: Ganyanka  Matele  na Edward Magafu wameipongeza serikali kwa jitihada za kupambana na matumizi ya zana haramu za uvuvi ikiwa ni njia ya kutokomeza uvuvi haramu hapa nchini. 
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
No comments: