LIVE STREAM ADS

Header Ads

MCHANGA WA MADINI WAWAPONZA VIONGOZI WENGI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

#BMGMtandaoni
Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuachia madaraka kwa kushindwa kusimamia suala la mchanga wa dhahabu unaosafirishwa kwenye makontena kwenda nje ya nchi.

Amemtaka waziri huyo kujitathimini na bila kuchukua muda mrefu aachie madaraka kutokana na suala hilo.

Rais Magufuli amesema hayo baada ya kamati ya kwanza iliyokuwa ikichunguza suala la mchanga kwenye makontena hayo kukabidhi ripoti yake hii leo, Ikulu jijini Dar es salaam.

Kamati hiyo ya wataalamu wa Jiolojia na uchambuzi wa kisayansi iliyoundwa Machi 29 mwaka huu, ilichunguza aina ya madini yaliyopo, kiasi na viwango vya ubora.

Akikabidhi ripoti hiyo, Profesa Mruma amesema uchunguzi huo umebaini uwepo wa madini ya kiasi cha kati ya Sh.829.4 bilioni mpaka 1.439 Trillion kwa makontena yote 277.

"Licha ya uchunguzi uliofanywa kupitia makontena haya, tumegundua uwepo wa aina nyingi zaidi za madini ambayo hayakuwa yakijulikana na haya yamekutwa na thamani ya kati Sh129.5 bilioni mpaka 261 bilioni," amesema Profesa Mruma.

No comments:

Powered by Blogger.