PUMZIKA KWA AMANI MZEE NGOSHA.

Rais John Magufuli, alipomtembelea mzee Kanyasu, akiwa hospitalini kabla ya mauti kumkuta.
#BMGHabariMchoraji wa Nembo ya Taifa, mzee Francis Kanyasu amefariki duniani, katika hospitali ya taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mzee Kanyasu maarufu kwa jina la Ngosha amefariki dunia jana majira ya saa mbili usiku baada ya hali yake kubadilika ghafla ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa na umri wa miaka 89.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Uumma, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, amethibitisha kufariki kwa mzee Ngosha aliyefikishwa hospitalini hapo mei 25 mwaka huu akitokea hospitali ya amana.
Awali mzee Ngosha alikuwa akipatiwa matibabu na serikali baada ya taarifa zake kusambaa kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kwamba anataabika mitaani kabla ya kupewa hifadhi na msamalia mwema.
No comments: