LIVE STREAM ADS

Header Ads

WASANII WA MAIGIZO WAMWANGUKIA DC WA GEITA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mwenyekiti wa chama cha Wasanii Mkoani Geita ,Bi Rose Michael(ROSE BINANZA)Akizungumza na waandishi wa habari juu ya kutokupatiwa ushirikiano na Mkuu wa Wilaya ya Geita.

Sagari Mganga ni Moja kati ya wasanii wa maigizo akisisitiza na kuomba  kupatiwa sapoti wao kama wasanii na wadau mbali mbali waliopo Wilayani na Mkoani Geita.








Chama cha wasanii wa Maigizo Wilaya na Mkoa wa Geita kimejitokeza hadharani na kuomba kupatiwa mchango (sapoti) kutoka kwa wadau  na viongozi Waliopo Mkoani Humo lengo likiwa ni kutangaza kazi ambazo wanazifanya pamoja na Kuutangaza Mkoa kwa ujumla.

Hayo yamekuja ni baada ya kuwepo kwa taarifa ambazo wao kama chama wamedai kuwa zimewasikitisha na kuwavunja moyo kutokana na kutokupewa ushirikiano na mkuu wa Wilaya ya Geita pindi wanapomuhitaji kwenye kazi zao, na mwisho wa siku wameshuhudia Mkuu wa Wilaya hiyo akiandika barua za kuunda kamati kwa ajili ya uzinduzi wa Filamu ambayo imechezewa Mkoani humo na wasanii kutoka Zanzibar huku wao wakibakia kukosa ushirikiano kutoka kwenye ngazi ya Wilaya.

Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii Mkoani Humo,Rose Michael amezungumza na Maduka online na kusema kuwa kumekuwepo na baadhi ya viongozi kutokuwapa ushirikiano, na mwisho wa siku kuwepo kwa matabaka kwa baadhi ya wasanii wanaotoka nje ya Wilaya kupatiwa ushirikiano wakati wao  wanapowafuata kuwaomba msaada wamekuwa wakiwakwepa.

“Mimi kama mwenyekiti wa chama cha wasanii tumesikitishwa sana na mkuu wetu wa wilaya ya Geita kushindwa kutupatia ushirikiano na mwisho wa siku kutoa ushirikiano huo kwa wasanii kutoka nje sisi ndio wa kwanza kuitangaza Geita ndani na nje ya nchi leo hii kama tunahitaji sapoti kwa viongozi wetu wa serikali wanatukwepa ni wapi tutakimbilia, nadhani ni muhimu kwa viongozi kupenda vya kwao kwanza kabla ya vitu vya nje kama watashindwa kutushika mkono na wakawabeba wasanii wa  nje hii ni swala la ajabu sana leo hii Wazanzibari watasaidia nini kwenye Wilaya yetu ya Geita na ndio maana tunapoomba msaada kwenye mgodi tumekuwa tukinyimwa na kupigwa kalenda lakini wa nje wakija wanasaidiwa kwa uharaka zaidi kiukweli imetusikitisha sana”Alisema Rose.

Hata hivyo moja kati ya wasanii ambao wamezindua Filamu yake inayojulikana kwa jina la WALIMWENGU,Michael Kapaya ameelezea kuwa yeye pia ni moja kati ya watu ambao aliahidiwa na mkuu wa Wilaya kufika kwenye shughuli yake ya uzinduzi lakini baada ya siku kuwa zimebakia chache alimwambia kuwa hataweza kufika kutokana na kutingwa na majukumu ya kiserikali.

“Sisi tunalia kwa ajili yake kwa sababu ya kutokupewa sapoti na watu ambao wapo serikalini naomba watambue kuwa sanaa ni ajira mimi namuomba mkuu wa Wilaya akae chini afikirie anatusaidiaje sisi wasanii ambao tu katika Wilaya yake tunateseka sana mwisho wa siku huwa tunajifikiria kukataa tamaa na hizi kazi lakini basi tu kwa sababu ndio ajira zinazotuweka mjini”Alisema Kapaya

Maduka Online imezungumza na Mkuu wa wilaya hiyo,Mwl Herman Kapufi ambapo ametolea maelezo malalamiko hayo na kusema kuwa yeye hana tatizo  lolote na wasanii.

“Ni  kwamba tatizo lililotokea mwaka jana kwenye shughuli ya Miss Geita walikuja kuniomba kuwa niwasaidie kupata ufadhili kutoka Mgodi wa dhaahabu wa Geita (GGM) na mimi niliwaombea  na walifanikisha kupatiwa shilingi milioni Kumi (10) lakini fedha hizo ambazo waliomba zilileta ugomvi na kushindwa kufanya lengo ambalo lilikusudiwa hali hiyo ilipelekea kunivunja  moyo maana kama kwa jambo dogo wameshindwa kuwa waaminifu sidhani kama wanaweza kuwa waaminifu kwa mambo makubwa”Alisema Mh,Kapufi.

Kuhusu swala la kuwasaidia wasanii wa nje ya Wilaya ya Geita na kutokuwapatia msaada wao wa ndani Mkuu wa Wilaya amesema kuwa  msaada wa GGM umetoka kwa Bw ,Shayo yeye amefanya kazi ya kusambaza barua ni kutokana na kuombwa na Waziri wa Zanzibar wa michezo kupitia kwa aliyekuwa waziri wa sekta hiyo Mh,Nape Nnauye kuwapa msaada wa kupata wafadhili ambao watawasaidia kwenye uzinduzi wao.

Mh,Kapufi ameongeza kwa kuwashauri wasanii kuwa na umoja kutokana na kuwapo makundi ambayo yamekuwa yakiwagawa kwenye shughuli zao za sanaa huku akiwasisitiza kuwa na akauti pamoja na ofisi ambazo zitawasaidia kuwatambulisha.

IMEANDALIWA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE .


No comments:

Powered by Blogger.