LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAMIA WAFUNGULIWA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA INJILI JIJINI MWANZA

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

 Na George Binagi-GB Pazzo
Wakazi wa Jiji la Mwanza wakiwemo waumini wa dini mbalimbali wameendelea kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkubwa wa injili ulioandaliwa na kanisa la kanisa EAGT Lumala Mpya chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kukola.

Jana mamia ya wananchi walijitokeza kwenye mkutano huo unaofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza na kukutana na mlipuko mkubwa wa injili kutoka kwa watumishi wa Mungu akiwemo mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani chini ya huduma ya MORE International Ministry.

Aidha waimbaji Ambwene Mwasongwe, Mbilikimo Watatu, Samwel Lusekelo, Joseph Rwiza, Sam D, Havillah Gospel Singers na wengine wengi wameendelea kukonga nyoyo za wahudhuriaji kwenye mkutano huo.

“Maandalizi ya mkutano huu ni ya kuvutia, tuna majukwaa matatu makubwa, vyombo vya muziki wa injili vizuri na pia tunatoa zawadi mbalimbali ikiwemo vyakula na nguo kwa wanaohudhuria mkutano huu”. Alisema Mchungaji Dkt.Kulola na kuwahimiza watu wote kufika kwenye mkutano huo ili wakutane na nguvu ya Mungu na kufunguliwa.


Mkutano huo ulianza juzi jumatano Septemba 27 na utafikia tamati jumapili Oktoba Mosi, 2017 katika Uwanja wa Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza ambapo mamia ya wananchi waliokuwa wakiteswa na majini pamoja na magonjwa mbalimbali wanazidi kufunguliwa, na leo huduma ya maombezi inaanza mapema majira ya saa nne asubuhi na mkutano utaanza saa tisa alasiri hadi saa 12 jioni.
Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani akihubiri kwenye mkutano huo
Kushoto ni Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani akihubiri kwenye mkutano huo. Kulia ni mkarimani Max Kemy kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya
Jana wananchi walijitokeza kwa wingi kwenye maombezi katika mkutano huo
Watumishi mbalimbali wakiendelea kutoa huduma ya maombezi jana ambapo zaidi ya 20 walifunguliwa mapepo huku wengine wengi wakiponywa magonjwa mbalimbali
Mchungaji wa kanisa la kimataifa EAG Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola akiomba kwenye mkutano huo
Mwimbaji wa muziki wa injili Ambwene Mwasongwe kutoka Dar es salaam akihudumu kwenye mkutano ho
Wanafahamika kwa jina maarufu Mbilikimo kutoka Arusha wakihudumu kwenye mkutano huo
Lusekelo Samwel akihudumu kwenye mkutano huo
Joseph Rwiza akihudumu kwenye mkutano huo
Watumishi wa Mungu kutoka Marekani
Mwinjilisti Rojas Matias (katikati) kutoka Marekani akiwa na timu yake
Watumishi wa Mungu kutoka Marekani
Mchungaji Mercy Kulola (kushoto) akiteta jambo na Mama Kulola (kulia)
Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia) akiteta jambo na mwimbaji Ambwene Mwasongwe (kushoto)
Watumishi wa Mungu wakifuatilia mkutano
Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola (wa kwanza kulia) pamoja na wageni kutoka Marekani
Baada ya ibada, kanisa la EAGT Lumala Mpya kwa kushirikiana na wachungaji kutoka Marekani lilitoa zawadi kwa wananchi
BMG Habari, Pamoja Daima!

No comments:

Powered by Blogger.