MASHABIKI WA SIMBA SC MWANZA WAWAANDALIA WACHEZAJI NA VIONGOZI WA TIMU HIYO CHAKULA CHA USIKU
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Binagi Media Group
Msemaji wa Simba Haji Manara amesema timu hiyo haina mpango
wa kuachana na kocha wake mkuu Joseph Omogi na kukanusha uvumi mitandaoni kwamba kocha huyo
ametakiwa kushinda mechi tano zijazo, lasivyo atatimliwa.
"Simba bado ni timu bora chini ya kocha Omogi, na
niwaambieni tu kwamba Simba inamhitaji zaidi Omogi, kuliko Omogi anavyoihitaji
Simba". Alisema Manara huku akisisitiza kwamba hitaji la Simba msimu huu
ni kikombe na si vinginevyo.
Aliyasema hayo jana jijini Mwanza wakati akizungumza na
wanahabari kuhusu maandalizi ya timu hiyo iliyoweka kambi Jijini humo ikiwa ni
maandalizi ya kuelekea kwenye mchezo wa jumapili dhidi ya Stand United mkoani
Shinyanga ambapo alisema kikosi kiko vizuri na hakina majeruhi.
Baadaye mashabiki wa Simba SC Jijini Mwanza (Rock City Simba SC
Funs) waliwandalia wachezaji na viongozi wa timu hiyo chakula cha usiku ambapo Mwenyekiti wa mashabiki hao Bittony Mwakisu alisema
mashabiki wana imani na timu yao hivyo ipambane kuhakikisha inanyakua ubingwa
katika msimu huu.
Msemaji wa Simba SC, Haji Manara alizungumza mambo mengi
ikiwemo mikakati ya timu ambayo itaifanya kuwa timu bora na tajiri huku akisisitiza pia msimamo wa timu hiyo juu ya kocha Omogi.
Hafla hiyo ilifanyika Diamond Hotel.
Mmoja wa mashabiki wa Simba SC Jijini Mwanza, Filbert Kabago.
Mwenyekiti wa Rock City Simba SC Funs, Bittony Mwakisu akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Rock City Simba SC Funs, Bittony Mwakisu akizungumza kwenye hafla hiyo.
Msemaji wa Simba, Haji Manara akizungumza kwenye hafla hiyo.
BMG Habari, Pamoja Daima!
No comments: