Salamu za mbunge wa Nyamagana kwa Rais Magufuli
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Na Binagi Media Group
Rais Dkt.John Pombe Magufuli jana alianza
ziara ya kikazi ya siku mbili Jijini Mwanza ambapo alizindua daraja la juu la
watembea kwa miguu la Furahisha, kuzindua kiwanda cha vinywaji baridi cha
Sayona pamoja na kuwahutubia wananchi katika uwanja wa Mwatex.
Miongoni mwa viongozi waliopata fursa
ya kuwasilisha salamu zao mbele ya Rais Magufuli ni pamoja na mbunge wa jimbo
la Nyamagana, Stanslaus Mabula ambaye alifunguka mambo mengi ya kimaendeleo
yaliyofanywa katika uongozi wake.
Baadaye Rais Magufuli alizungumza na
wananchi na kusema kwamba amedhamiria kuibadilisha Tanzania kupitia mkakati
wake wa ujenzi wa viwanda ambao utaimarisha uchumi pamoja na kutoa ajira nyingi
kwa vijana huku akiwataka viongozi Jijini Mwanza kuungana pamoja kumaliza
miogogoro waliyonayo hii ikiwa ni baada ya kupata taarifa ya kukamatwa kwa Meya
wa Jiji la Mwanza, James Bwire, alipowasili kwenye uwanja wa ndege.
Bonyeza HAPA habari zaidi
No comments: