Haruna Moshi kuivusha African Lyon Ligi Kuu
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, BMG
Meneja wa
timu ya African Lyon Adam Kipatacho amesema anaamini mchezaji wao Haruna Moshi ataisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika
msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza
na majira jijini Mwanza Kipatacho alisema, Moshi ana nafasi kubwa katika kuisaidia timu hiyo, kwani umri
wake siyo mkubwa kama watu wanavyodhani wa kushindwa kusakata kabumbu.
Moshi katika
mchezo wa raundi ya pili ya ligi kuu uliowakutanisha na Alliance FC ya jijini Mwanza
aliifungia timu hiyo goli moja dakika ya nane, na kufanya hadi dakika tisini
kumalizika kutoka sare ya goli 1-1.
Mchezaji
huyo aliyewai kuichezea timu ya Moro United na Simba SC miaka kadhaa, ndiye
pekee aliyeweza kuifungia timu yake goli tangu kuanza kwa ligi msimu huu.
Alisema,
kuelekea mchezo wa raundi ya tatu dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa septemba Mosi katika uwanja wa
Kaitaba wamejipanga vizuri, anaamini wataibuka na point tatu hivyo kurejea Dar
wakiwa na point nne kutoka Kanda ya Ziwa baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza
waliocheza na Stand United ya mkoani Shinyanga.
"Mchezo
haukuwa mbaya sana tumeyapokea matokeo hayo kwa sababu sisi tulikuja kutafuta
point moja ndio lengo letu haswaa hivyo Kagera ndio tunaenda kumaliza gemu
tutarejea dar tukiwa na point 4," alisema Kipatacho.
No comments: