Wizara ya afya yahimizwa kuongeza miuda ugawaji dawa za minyoo na kichocho
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, BMG
Wizara ya
Afya kupitia mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewikKipaumbele (NTD),
imehimizwa kuongeza muda wa zoezi la ugawaji dawa za minyoo na kichocho ili
kufikia walengwa wengi.
Mratibu wa magonjwa
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,
Gisela Orasa amesema kuna changamoto mbalimbali zinazopelekea zoezi la ugawaji
dawa za kichocho na minyoo shuleni kutofanikiwa kwa asilimia mia ikiwemo ufinyu
wa siku.
Alisema zoezi
la ugawaji dawa limekuwa likifanyika kwa
siku moja ambapo kwa mwaka huu limefanyika Agosti sita, hali inayopelekea
kutofanikiwa kwa asilimia mia kwani walilenga kuwafikia wanafunzi 94,743 kutoka
shule za msingi 116 na waliomeza dawa ni
84,417.
"Kuna
baadhi ya wanafunzi hawakufika shuleni siku ya zoezi la ugawaji dawa za
magonjwa ya kichocho na minyoo kutokana na sababu mbalimbali ni bora wizara
husika ikaongeza siku angalau zikawa tatu ambapo mtoto ambaye
hakumeza siku ya kwanza atapewa siku ya pili au ya tatu”. Alisema Orasa.
Kwa upande
wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Dkt. Florian Tinuga alisema mkakati walionao katika
kudhibiti magonjwa hayo ni kuingiza kwenye bajeti ya wilaya ambapo kwa sasa
wanayapa kipaumbele kwani wanahitaji fedha za kutosha ili kuwafikia wananchi.
Alisema mwaka
ujao wataanza zoezi la uhamasishaji mapema
pamoja na kuweka mfumo mmoja
ambao utakuwa kwa shule zote zilizopo katika halmashauri hiyo kwa kukaa na
wazazi na kupendekeza ni namna gani watachangia chakula ili kufanikisha zoezi
hilo kwa asilimia mia na watoto wanameza dawa hizo.
No comments: