Ibungilo watinga robo fainali michuano ya Angeline Jimbo Cup wilayani Ilemela
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith
Ferdinand, BMG
Timu ya
Ibungilo imeendeleza kutoa kipigo baada ya kuifunga Nyamanoro goli 4-0 katika
mashindano ya Angeline Jimbo Cup msimu wa 2018/19 yanayoendelea kutimua vumbi
katika viwanja mbalimbali wilayani
Ilemela.
Katika
mchezo uliochezwa jana kwenye uwanja wa Kona ya Bwiru na kukutanisha timu
kutoka kundi A, ambapo Nyamanoro ilionekana kuzidiwa mashambulizi na hadi dakika
tisini walishindwa kutikisa nyavu za Ibungilo.
Timu ya
Ibungilo ilifunga magoli kupitia washambuliaji wake Said Said magoli matatu na
Didas Msafiri goli moja, hivyo kufanya timu hiyo kuongoza katika kundi hilo kwa
kuwa na jumla ya pointi kumi huku wakishinda mechi tatu na sare moja.
Akizungumza baada
ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha wa Ibungilo Swala Daud alisema alishukuru
kwa matokeo aliyopata kwani mpaka sasa timu yake imefuzu kutinga hatua ya nane
bora (robo fainali).
Alisema timu
yake inafanya vizuri japo yapo mapungufu madogo ambayo atayafanyia kazi ili
kuweza kufuzu kuingia fainali na kuibuka mabingwa wa msimu huu kwani ndio lengo
huku aliwashukuru mashabiki wa timu hiyo na kuwaomba waendelee kuiunga mkono
kwani hatua inayofuatia ni ngumu zaidi na watakutana na mabingwa wa hatua ya
makundi.
Katika mchezo
mwingine uliochezwa katika uwanja wa Buswelu, timu ya Kata ya Mecco imeibuka na
ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Kahama kupitia kwa washambuliaji wake Paul
Charles, Sylvester Godfrey na Lucas Anderson huku Kahama wakipata goli la
kufutia machozi kupitia kwa Legan Legan.
No comments: