Inshu ya wizi wa mitihani imefika kwenye baraza la madiwani Ilemela
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, BMG
Jumla ya watahiniwa ,8904 katika
Halmashauri ya wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, wanatarajiwa kufanya mtihani wa
taifa darasa la saba wa kuhitimu elimu ya msingi unaotarajiwa kufanyika Septemba
03 hadi 06, 2018.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, John
Wanga aliyasema hayo kwenye kikao cha robo ya nne ya mwaka 2017/18 cha baraza
la madiwani na kuongeza kwamba kati ya watahiniwa 8,904
wavulana ni 4195 na wasichana ni 4,709 kutoka shule za msingi 107.
Alisema
Halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha hakuna vitendo vya udanganyifu kwenye
mtihani huo huku akisifu matokeo ya mtihani wa “MOCK” ambapo halmashauri hiyo
ilishika nafasi ya pili kimkoa.
Kwa upande
wake Naibu Meya wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa Kata ya Ilemela,
Willbard Kilenzi alisema kuna malalamiko na minong’ono kuhusu baadhi ya shule
za binafsi na serikali kufanya udanganyifu katika mitihani ya taifa ili ionekane
wanafanya vizuri hivyo ni vyema suala hilo likafanyiwa uchunguni na shule
zitakazobainika kufanya udanganyifu zichukuliwe hatua za kisheria.
No comments: