LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanaume Mwanza watambua umuhimu wa kupima VVU

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI), limewakutanisha wadau wa mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi VVU na Ukimwi mkoani Mwanza ili kujadili na kuweka mikakati ya kuongeza idadi ya wanajamii hususani wanaume wanaojitokeza kupima VVU ili kutambua hali zao.

Kikao cha wadau hao kutoka wilaya za Nyamagana, Ilemela, Sengerema, Ukerewe, Misungwi pamoja na Magu kimefanyika kwa siku mbili kuanzia Agosti 17, 2018 katika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.

Afisa Miradi (Huduma Unganishi kwa Jamii) kutoka shirika la AGPAHI mkoani Mwanza, Cecilia Yona amesema kikao hicho ni matokeo ya kikao kilichoketi mwezi Mei mwaka huu katika ukumbi wa Adden Palace Hotel Jijini Mwanza ambapo wadau wanaotoka katika vikundi vya kijamii (CBO) pamoja na waratibu wa VVU na Ukimwi ngazi za wilaya walikubaliana kuwafikia wananchi wengi hususani wanaume kwa ajili ya kuwaelimisha kuhusu VVU na Ukimwi.

Amesema utekelezaji wa maazimio ya kikao hicho umeonyesha mwazo mzuri ambapo idadi ya wanaume waliojitokeza kupima afya zao imeongezeka huku waliokutwa na maambukizi wakionyesha utayari wa kuanza kutumia dawa za kufubaza maambukizi ya VVU.

Kwa pamoja washiriki wa kikao hicho wamekubaliana kutumia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, mikusanyiko ya hadhara, nyumba za ibada pamoja na Vituo va Tiba na Matunzo ili kufikisha elimu kuhusu VVU na Ukimwi lengo likiwa ni kuhakikisha jamii hususani wanaume inatambua umuhimu wa kupima afya zao pamoja na kuwarejesha kwenye tiba baadhi ya wateja ambao wameacha matumizi ya dawa za kufubaza maambukizi ya VVU.

Takwimu za maambukizi ya VVU mkoani Mwanza zinaonyesha kuongezeka kutoka asilimia 4 miaka miwili iliyopita hadi asilimia 7.2 hivyo juhudi zinazofanywa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa serikali ya Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control (CDC) zinaleta taswira chanya katika kupambana na ongezeko la maambukizi hayo.
Afisa Miradi (Huduma Unganishi kwa Jamii) kutoka shirika la AGPAHI mkoani Mwanza, Cecilia Yona akizungumza kwenye kikao hicho
Washiriki wa kikao hicho wakimsikiliza Afisa Miradi (Huduma Unganishi kwa Jamii) kutoka shirika la AGPAHI mkoani Mwanza, Cecilia Yona

PIA SOMA Shirika la AGPAHI lafanya mkutano na wadau wa Ukimwi mkoani Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.