LIVE STREAM ADS

Header Ads

Michuano ya Angeline Cup 2018 yazidi kupamba moto wilayani Ilemela

 Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, BMG

Michuano ya Angeline Cup 2018 imeendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali wilayani Ilemela ambapo jana timu ya Kata ya Ibungilo iliichabanga timu ya Kata ya Pasiansi bao 3-1.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Kona ya Bwiru ukihusisha timu kutoka kundi A, Ibungilo walipata magoli yao kupitia kwa washambuliaji wake Michael George aliyefunga goli moja na Said Said aliyepachika magoli mawili.

Mchezo mwingine uliochezwa wenye uwanja wa Buswelu na ukikutanisha timu za kundi  B ambapo Nyakato ilitoa kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Kahama kupitia mshambuliaji wake Hamada Mtegeta.
Timu ya Shibula imeilaza Kayenze kwa magoli 3-2 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa shule ya msingi Bugongwa na kukutanisha timu kutoka kundi D.

Wakati huo huo Nyasaka imeiondoka na pointI tatu baada ya kuichapa Kawekamo goli 2-1 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sabasaba ukikutanisha timu kutoka kundi C.

Ikumbukwe kuwa mashindano hayo yalizinduliwa Agosti 11, 2018 ambapo yameandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Angeline Mabula yakishirikisha timu 19 kutoka Kata zote za wilayani Ilemela kwa lengo la kuibua vipaji kwa vijana.

No comments:

Powered by Blogger.