RC Mwanza ameguswa inshu ya wanafunzi kusomea nje
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa
Mwanza Mhe.John Mongella ameguswa na suala la upungufu wa vyumba vya madarasa
katika shule ya msingi Nkumba iliyopo wilayani Sengerema na kuungana na wananchi
kuchangia ujenzi wa vyumba vitatu vya madarsa shuleni hapo.
RC Mongella
amefanya ziara katika shule hiyo akiambatana na viongozi mbalimbali akiwemo
Mkuu wa Wilaya Sengerema, Mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema, Kamati ya Ulinzi
na Usalama Mkoa Mwanza na kuendesha harambee ya papo kwa hapo ili kiufanikisha
ujenzi huo.
Katika
harambee hiyo, shilingi 710,000 zilipatikana pamoja na ahadi ya mifuko minane
ya saruji, tripu mbili za mchanga, debe nne za mpunga, kuku watatu pamoja na
debe moja la mchembe lengo likiwa ni kuwanusuru zaidi ya wanafunzi 200
wanaosomea nje.
Pia RC Mongella
amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Sengerema ikiwemo mradi wa
kisima Kisoli, ghala la chakula Isole, ujenzi wa maabara, jengo la upasuaji, chumba
cha kuhifadhia maiti, nyumba ya mtumishi, wodi ya baba, mama na mtoto katika
Kituo cha Afya Kagunga.
Vyumba vya madarasa vinavyojengwa katika shule ya msingi Nkumba wilayani Sengerema
Ghala la chakula katika Kijiji cha Isole
No comments: