LIVE STREAM ADS

Header Ads

Misungwi wapongezwa ushiriki wa Maonesho ya Nane Nane

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Antony Bahebe (kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Antony Nchimani (kushoto) ambaye ni Katibu Meneja wa Chama cha Msingi cha Ushirika Mwajombo wilayani Misungwi.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Antony Bahebe ametembelea mabanda la halmashauri hiyo kwenye Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Ziwa Maghabiri na kuvutiwa na elimu inayotolewa kwa wananchi.

Maonesho hayo yanayoshirikisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera yanafanyika katika uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza kuanzia Agosti Mosi hadi Agosti 08, 2018 yakijumuisha maonesho ya bidhaa za kilimo, ufugaji na uvuvi.

Bahebe amevutiwa na elimu inayotolewa kwenye mabanda ya halmashauri ya Misungwi hususani kuhusu kilimo cha mazao mbalimbali ikiwemo pamba, ufugaji pamoja na usindikaji wa mazao mbalimbali.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Antony Bahebe (kushoto) akitoa pongezi kwa kikundi cha "Upendo Group" kinachozalisha mvinyo asilia
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Antony Bahebe (kulia) akisikiliza ufafanuzi wa bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha "Juhudu Group" kutoka Kata ya Ngudama Misungwi ambapo alitoa pongezi kwa kikundi hicho na kuhimiza kitoe mafunzo ya uzalishaji wa bidhaa za mikono kama vyungu kwa wananchi wengine
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Antony Bahebe akiwa ameshikilia mhogo. Aina hii ya mbegu bora ya mhogo inapatikana kwenye mabanda ya halmashauri ya Misungwi
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Antony Bahebe akijionea mabanda ya wafugaji

No comments:

Powered by Blogger.