Waziri wa Kilimo awahakikishia soko wasindikaji wa zao la pamba
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.
Na Mathias
Canal, WK-Mwanza
Waziri wa
Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amewahakikishia wanunuzi na wasindikaji wa zao la
Pamba kuendelea kununua na kusindika pamba kwa wingi kutoka kwa wakulima kwani
soko la zao hilo kwa sasa limeimarika kwa kiasi kikubwa.
Waziri
Tizeba ametoa kauli hiyo juzi tarehe 9 Agosti 2018 wakati akizungumza kwenye
mkutano wa kazi kati ya wanunuzi
/wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX)
ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Mwanza Hoteli Jijini Mwanza.
Katika
mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwapatia uelewa wanunuzi wa zao la Pamba Mhe
Tizeba alisema kuwa kuna njia mbadala zaidi ya waliyonayo sasa ya kuuza Pamba
yao katika soko la bidhaa ambapo bidhaa hushindanishwa kutokana na ubora wake
kwa wanunuzi walio wengi Duniani.
Alisema
kuingia kwenye ushindani wa soko ni miongoni mwa njia muhimu na madhubuti kwao
kwani itaongeza thamani ya zao hilo hivyo kuwa na kipato kikubwa
kitakachoongeza tija na mafanikio ya kipato.
Tanzania
Merchantile Exchange (TMX) inawakutanisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa kwa
pamoja na kwa wingi ili washindane katika bei jambo ambalo litawafanya wauzaji
kuuza bidhaa zao kwa kiasi kizuri cha fedha na kupelekea kupata bei nzuri.
Katika
mkutano huo Mhe Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba aliwataka wanunuzi hao
kujifunza namna ambavyo soko la bidhaa Tanzania Merchantile Exchange (TMX)
linafanya kazi Kwa kupeleka kiasi cha Pamba kilichozidi kutokana na mkataba
walioingia na wanunuzi wao Nje ya nchi ili kujionea manufaa yaliyopo.
Hata hivyo
Mhe Tizeba aliwataka wanunuzi hao kuendelea kununua Pamba kwa wakulima bila
wasiwasi wowote, kwani soko la bidhaa litaweza kutumika kwa manufaa makubwa
kuuza Pamba yao na kumhakikishia mkulima soko.
Alisema kuwa
Katika ngazi ya uzalishaji ni muhimu sana ubora wa pamba ukaimarishwa ili soko
la bidhaa liweze kufanya kazi kwa ufanisi. Aidha, Mhe
Tizeba ameilekeza TMX kukutana na kampuni zinazonunua pamba mmoja mmoja ili
kubaini kampuni ambazo zitaweza kuanza msimu huu kutumia soko la bidhaa.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini
Wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na waendeshaji
wa soko la bidhaa nchini Tanzania Merchantile Exchange (TMX) wakimsikiliza kwa
makini Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba
No comments: