LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kiongozi wa Mwenge ataka mradi wa mzani Ilemela ukamilike haraka

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Charles Kabeho amemwagiza mkandarasi kampuni ya M/S Great Lakers ya Mwanza kuhakikisha anakamilisha kwa wakati mradi wa ujenzi wa mizani Mwaloni Kirumba.

Kabeho alitoa kauli hiyo jana kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo unaojengwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa gharama za shilingi milioni 293, 268, 739 ikiwa ni fedha za ndani.

Alisema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kupunguza malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara pamoja na kuongeza mapato ya serikali kuu na Manispaa ya Ilemela.

Taarifa ya mradi huo inaonyesha utekelezaji ulianza Novemba 11, 2017 na ulitarajiwa kukamilika Februari 22, 2018 lakini haukukamilika kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kubadilishwa eneo la mradi na hivyo kusababisha kuongezeka kwa kazi kutokana na aina ya udongo.
Miradi mingine iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni pamoja na ufunguzi wa karakana ya mafunzo ya ufundi wa umeme wa viwandani katika chuo cha VETA Mwanza uliogharimu shilingi milioni 320,398,091.27, ufunguzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Buswelu uliogarimu milioni 150,888,910, uwekaji jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Zahanati ya Lukobe uliogharimu milioni 46,615,000.

Pia uwekaji jiwe la msingi kwenye ujenzi wa shule ya msingi Tarajali (Bugogwa B) ambao hadi sasa umegharimu shilingi milioni 85, 872,000, ujenzi wa ofisi ya Kata Pasiansi uliogharimu shilingi milioni 50,189,000 na ujenzi wa barabara ya Kabuhoro-Ziwani yenye urefu wa kilomita 1.5 inayojengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya Gemen Engineering kwa shilingi milioni 916,812,210.

PIA SOMA Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa atoa ujumbe mzito Ilemela

No comments:

Powered by Blogger.