LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko atatua mgogoro baina ya wawekezaji wawili mkoani Morogoro

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Mashaka Biteko akisikiliza maelezo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya Buddha Mining and Explorers wakati wa kusikiliza na kutatua mgogoro baina ya kampuni hiyo na kampuni ya Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd baada ya kufanya ziara katika mgodi wa uchimbaji madini/ mawe ya marumaru Mabo (Mable) mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Mashaka Biteko akitoa maamuzi baada ya kikao kifupi cha utatuzi wa mgogoro baina ya kampuni ya Buddha Mining and Explorers na kampuni ya anzania Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini akizungumza baada ya Naibu Waziri wa Madini Mwl. Doto Biteko kutembelea machimbo ya mabo mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Mashaka Biteko (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa mampuni ya Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd, Alston Zhiling Yi (kulia). Kampuni hiyo inajishughulisha na uchimbaji wa mawe/ madini ya ujenzi aina ya mable katika Kijiji cha Maseyu Kata ya Gwata mkoani Morogoro.
Sehemu ya mitambo ya kuchakata madini ya mabo katika eneo la mgodi wa madini hayo unaomilikiwa na kampuni ya Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd iliyopo katika Kijiji cha Maseyu mkoani Morogoro.
Baadhi ya malighafi zitokanazo na madini ya mabo (Mable) zinazotengenezwa na kampuni ya Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd mkoani Morogoro. Madini haya hutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo "Tiles".

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Mashaka Biteko ametatua mgogoro baina ya kampuni ya Buddha Mining and Explorers na kampuni ya Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd zilizokuwa ziking’ang’ania eneo moja kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini katika Kijiji cha Maseyu Kata ya Gwata mkoani Morogoro.

Awali kampuni ya Buddha Mining and Explorers iliomba leseni kwa ajili ya kufanya utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo hilo na baadae kampuni ya Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd ikabaini uwepo wa madini ya mabo katika eneo hilo na kuanza shughuli zake bila kuwa na leseni hatua ambayo iliibua mvutano baina ya kampuni zote mbili.

Alhamisi Oktoba 11, 2018 Naibu Waziri Biteko alikutana na pande zote mbili, kampuni ya Buddha Mining and Explorers ilikubali kuachia eneo hilo na hivyo kampuni ya Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co. Ltd kutakiwa kuomba rasmi leseni ya uchimbaji madini ya mabo ili ifanye shughuli zake kihalali na kulipa kodi zote stahiki.


SOMA>>>Serikali yasisitiza msimamo wa kuufunga mgodi wa kokoto wilayani Bagamoyo

No comments:

Powered by Blogger.