Dkt. Tizeba awataka wakulima wa pareto kujiunga na mfumo wa ushirika
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akikagua kiwanda cha Pareto Mafinga (PCT) kilichopo mamlaka ya Mji wa Mafinga.
Na Mathias Canal-WK,
Mufindi-Iringa
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) amewataka
wakulima wa Pareto kote nchini kujiunga na mfumo rasmi wa vyama vya msingi vya
ushirika.
Dkt Tizeba alitoa mwito huo jana wakati akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo
kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika
muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa.
Alisema kuwa ushirika ni dhana ya kuleta maendeleo kwa
kushirikiana ambapo dhana hiyo imefanikiwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi na
kijamii katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita.
“Kutokana na changamoto mbalimbali zilizoikumba sekta hii ya
ushirika watu wengi wamekosa imani na vyama hivi na baadhi ya vyama vimeshindwa
kufanya kazi vizuri hivyo nawahakikishia serikali inayoongozwa na Rais Dkt John
Pombe Magufuli imerejesha nidhamu kwenye ushirika” Alikaririwa Dkt Tizeba na
kuongeza kuwa;
Alisema kuwa Ushirika maana yake ni muungano wa watu ambao
wanafanya kazi pamoja kwa hiari ili kufanikisha mahitaji yao ya kiuchumi,
kijamii na kiutamaduni kupitia shughuli ya biashara inayomilikiwa kwa pamoja na
kudhibitiwa kidemokrasia. Ushirika unazingatia maadili ya kujisaidia wenyewe,
jukumu binafsi, demokrasia, usawa na mshikamano.
Wanachama wa Ushirika wanaamini katika misingi ya uaminifu,
uwazi, uwajibikaji kwa jamii na kuwajali wengine. Muundo wa Ushirika kwa ujumla
unategemea uimara wa chama cha msingi cha Ushirika, hivyo kuna umuhimu wa
kuhakikisha vyama imara vya msingi vinaanzishwa.
Wakulima wa Pareto katika Mikoa ya Nyanda za juu Kusini na
maeneo yote nchini wanapaswa kulima kwa wingi zao hilo ili waweze kuinua kipato
chao na kuondokana na umaskini kutokana na kuwepo kwa uhakika wa soko la zao
hilo.
Aidha, Waziri Tizeba amesimamisha utendaji kazi wa Wakala wa
ununuzi wa Pareto Wilayani Mufindi Ndg Nilbet Kabonge badala yake amemtaka
mwenyekiti wa kijiji kuitisha mkutano wa kijiji ili kuchagua wakala mwingine
atakayesimamia maslahi ya wakulima.
“Tena Mkurugenzi wa Halmashauri unapaswa kuhakikisha kuwa
unanunua mzani maalumu kwa ajili ya kupima ubora wa zao la Pareto kwani kufanya
hivyo kutaondoa udanganyifu wa muda mrefu kwenye zao hili” Alisema.
Kadhalika, aliutaka uongozi wa Wilaya ya Mufindi na uongozi
wa Mkoa wa Iringa kusimamia ipasavyo upimaji wa ubora wa zao la Pareto ili
kuepusha wizi na udanganyifu kwa wakulima wanaouza Pareto yao kupitia mawakala
wenye vipimo ambavyo havijathibitishwa na wakala wa vipimo nchini.
Pareto ni moja kati
ya zao ambalo hulimwa Tanzania, na huwa ni zao jamii ya ua ambalo hutumika
kutengenezea dawa za kuuwa wadudu shambani (insecticide) hujulikana kama
pyrethtin.
No comments: