Kongamano la ajira binafsi lafanyika mkoani Morogoro
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, akifungua kongamano la siku moja la ajira binafsi mjini Morogoro juzi, lililoandaliwa na Taasisi ya WICOF inayojishughulisha na masuala ya kijamii hususani, walemavu na watoto mkoani humo .
Washiriki wa kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WICOF, Mwajabu Dhahabu akimkabidhi zawadi ya picha baba yake Mzee Dhahabu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Gairo.
Kongamano likiendelea.
Mtoa mada Mogani Isdori akitoa mada kuhusu ulipaji kodi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akitoa mada kuhusu matumizi ya mitandao.
Mwanachuo cha Jordan cha mjini Morogoro, Aviva Chrispin akiuliza swali.
Mjasiriamali, Neema Heri akitoa ushuhuda wa mafanikio yake.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, Dk.Suleiman Rashid akitoa mada kuhusu umuhimu wa vifungashi kwenye Tangaza na kuongeza thamani ya bidhaa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza katika kongamano hilo akizungumzia umuhimu wa vifungashio na kuongeza thamani ya bidhaa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa kongamano hilo, DC Mchembe pamoja na watoa mada.
Mjasiriamali, Sara Ngonyani akitoa mada.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Mwajabu Dhahabu, akihutubia.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, akimkabidhi zawadi ya saa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo.Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WICOF, Mwajabu Dhahabu akimkabidhi zawadi ya picha baba yake Mzee Dhahabu.
Picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa katika picha ya pamoja na vijana walioshiriki katika kongamano hilo.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Gairo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WICOF.
Na Dotto Mwaibale, Morogoro
WANAWAKE
nchini wametakiwa kuthubutu, kuwa wavumilivu na wabunifu ili waweze kuinuka
kiuchumi.
Mwito huo
umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe mjini Morogoro juzi wakati
akifungua kongamano la siku moja la ajira binafsi lililoandaliwa na Taasisi ya
WICOF inayojishughulisha na masuala ya kijamii hususani, walemavu, watoto na
wazee mkoani Morogoro.
"Ili
mjikomboe kiuchumi mnatakiwa kuthubutu, kuwa wavumilivu nawabunifuna uiunga
katika vikundi vya ujasiriamali muweze kupata mikopo nakufanyashughuli
mbalimbali za biashara" alisema Mchembe.
Alisema
dhana ya 50 kwa 50 kati ya wanaume na
wanawake si kuosha vyombo bali ni mwanamke kuweza kufanya kazi za uzalishaji
mali kama wanavyofanya wanaume na kumiliki ardhi.
Akizungumza
wakati akitoa mada katika kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Trumark, Agnes Mgongo aliwataka wanawake hao kutumia mitandao ya kijamii kwa
maufaa badala ya kuitumia kwa masuala yasiyo na tija.
"Jamani
wanawake wenzangu tutumie simu zetu kwa ajili ya maendeleo, kama kupeana
taarifa, kutafuta masoko ya bidhaa zetu na si vinginevyo" alisema Mgongo.
Akitoa
zawadi ya pekee katika kongamano hilo alisema kwa kutambua umuhimu wa mtoto wa
kike Shule ya John The Baptist Girls High School imetangaza fursa ya kusomesha
bure wanafunzi watatu wa kidato cha
kwanza na watatu wengine hadi cha nne kwa mwaka 2019.
Alisema
anachotakiwa kufanya mwanafunzi ni kufika shuleni hapo siku yoyote ndani ya
mwezi wa oktoba 2018 kwa ajili ya kufanya mtihani wa kuchuana na kuwa fursa
hiyo imetolewa na Mfuko wa Ndibalema John Mayanja Memorial Scholarship.
Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi hiyo, Mwajabu Dhahabu alisema kuwa kongamano hilo lenye
lengo la kuwajengea uwezo ajira binafsi watoto wa kike ni la kwanza tangu
kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka jana.
Alisema
kufanyika kwa kongamano hilo ni maandalizi ya kuelekea katika maadhimisho ya
siku ya mtoto wa kike duniani yatakayofanyika hivi karibuni.
Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu Anthony Mtaka akizungumza katika kongamano hilo alisema serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli imeweka mazingira mazuri ya
kuwasaidia wajasiriamali na kuwa imetenga fedha
kwa ajili ya kuwakopesha hivyo akato mwito kwa wajasiriamali hao
kuongeza thamani ya bidhaa zao kwa kuziweka katika vifungashio vilivyobora.
Katika hatua
nyingine Mtaka aliipongeza kampuni ya Trumark kwa kazi kubwa inayoifanya ya
kuwasaidia vijana kuzitambua fursa za
maendeleo na akatoa mualiko kwa wajasiriamali hao kwenda Simiyu kwenye
maonyesho ya viwanda vidogo vidogo (SIDO) yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23
hadi 28.
Kongamano
hilo lilihitimishwa kwa makundi mbalimbali pamoja na watoa mada kupata zawadi
na vyeti vya ushiriki.
Kongamano la ajira binafsi lafanyika mkoani Morogoro
Reviewed by BMG Media
on
October 09, 2018
Rating: 5
Tags :
HABARI PICHA
No comments: