DC Misungwi aingilia kati mgogoro wa wachimbaji wadogo wa madini
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Mangazo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa
Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, Mhe. Juma Sweda ameagiza kupitiwa upya mkataba
baina ya kikundi cha wachimbaji wadogo wa dhahabu Nyabayombe kilichopo katika
Kijiji cha Lubili pamoja na Mwekezaji Seif Mahumbi baada ya kuibuka mgogoro wa
kimaslahi.
Mhe. Sweda
aliyetembelea machimbo hayo wiki iliyopita, alisema hatambui mkataba huo ambao
unampa mwekezaji haki ya asilimia 70 ya mauzo ya dhahabu baada ya kusababisha
mvutano wa kimaslahi baina ya kikundi hicho na ushirika wa wachimbaji wadogo wa
dhahabu wa Misungwi Mining Corperative Society Limited (MIMICOSO) uliokuwa na
makubaliano ya uchimbaji pamoja na kikundi hicho cha Nyabayombe.
Ilielezwa kwamba chimbuko la mgogoro huo ni baada ya kikundi cha Nyabayombe kinachomiliki
leseni 16 za uchimbaji dhahabu kuzuia ushirika wa MIMICOSO kuendelea na
shughuli zake kulingana na makubaliano yaliyokuwepo baada ya kuingia ubia mwingine
na mwekezaji Mahumbi.
Baadhi ya
wanachama wa kikundi hicho cha Nyabayombe waliwatupia lawama viongozi wao kwa
kusababisha mgogoro huo baada ya kuingia makubaliano na mwekezaji ambayo wao
hawayatambui huku wakimshukuru DC Sweda kwa kwa kutotambua mkataba huo na
kuwaruhusu kuendelea na shughuli zao.
Mwakilishi
wa Afisa Madini Mkazi mkoa Mwanza, Ndembi Nkingwa aliwataka wamiliki wa leseni za
uchimbaji madini kuzingatia sheria wakati wa kuingia ubia na wawekezaji ili
kuondokana na migogoro isiyo ya lazima.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: