LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali ya Ireland yaridhishwa na mapambano ya Ukatili Misungwi

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo
Serikali ya Ireland imepongeza juhudi za kupambana na Ukatili wa Kijinsia katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, na kuahidi ushirikiano zaidi ikiwemo kuendelea kufadhili miradi mbalimbali wilayani humo.

Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania, Adrian Fitzgerald aliyasema hayo Oktoba 29, 2018 kwenye mdahalo wa kupinga viashiria vyote vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake uliofanyika Kata ya Igokelo wilayani Misungwi.

“Nimefurahi kuona fedha za walipa kodi wa Ireland zinatumika vizuri hapa Misungwi hivyo serikali ya Ireland itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo hapa Misungwi”. Alisema Fitzgerald.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Misungwi, Katibu Katawala wilayani humo Petro Sabatho alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo haitamvumilia yeyote atakayejihusisha na ukatili wa kijinsia hususani mimba na ndoa za utotoni kuwataka wazazi kufichua taarifa za aina hiyo ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema wilaya ya Misungwi imekuwa wilaya ya mfano kwa kutekeleza vyema mkakati wa kupambana na ukatili wa kijinsia na hivyo kuwapongeza wanaharakati, madiwani pamoja na watendaji mbalimbali kwa ushirikiano wao.

Halmashauri ya wilaya Misungwi kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KVULINI la Jijini Mwanza inaendesha kampeni ya kupambana na Ukatili wa Kijinsia kwa watoto na wanawake wilayani humo kwa ufadhili wa shirika la watu wa Ireland (Irish Aid).
Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye mdahalo huo.
Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania, Adrian Fitzgerald
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, ACP. Jonathan Shanna alisema jeshi hilo halitasita kuwashughulikia wale wote wanaojihusisha na ukatili wa kijinsia hivyo wenye tabia hiyo waache mara moja.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Mwanza akiwasilisha salamu zake kwenye mdahalo huo
Katibu Katawala wilayani humo Petro Sabatho akizungumza kwenye mdahalo huo na kuonya baadhi ya waalimu kuacha tabia ya kujihusisha na vitendo vya mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi na kwamba sheria kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika.
Afisa Program shirika la Kivulini, Eunice Mayengelea akiongoza mdahalo huo
Watoto wakiwasilisha ujumbe wa kupambana na Ukatili wa Kijinsia kwa njia ya ngojera.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.