LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkuu wa Mkoa Geita adhihirisha ubora wake mbele ya Waziri Mkuu

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Robert Gabriel amedhihirisha ubora wake mbele ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa baada ya kufanikisha maonesho ya kwanza ya Teknolojia ya Uzalishaji Dhahabu kwa Maendeleo ya Kijamii na Uchumi wa Viwanda.

Akizungumza kwenye kilele cha maonesho hayo jana Septemba 30, 2018 Mhe. Gabriel alisema huo ni mwanzo wa kimapinduzi ya Geita mpya ya dhahabu na kwamba atahakikisha anasimamia vyema fedha za maendeleo ya jamii zinazotolewa na makampuni ya uchimbaji madini akibanisha kwamba fedha hizo zimesaidia ujenzi wa Zahanati na kufikia asilimia 93 kutoka asilimia 23.

Naye Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa hakusita kutoa pongezi za dhati kwa Mhe. Gabriel kutokana na utendaji kazi wake ambapo alimhimiza aendelee na kasi hiyo hiyo. 
Mkuu wa Mkoa Geita, Mhe. Robert Gabriel akizungumza kwenye maonesho hayo
Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Robert Gabriel (kulia) akimkabidhi zawadi maalum mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwa kutambua mchango wake katika sekta ya madini
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali
Tazama hapa chini BMG Online Tv

SOMA>>>Waziri wa Madini aibana GGM, atoa siku 30 za mwisho

No comments:

Powered by Blogger.