Waziri wa Madini aibana GGM, atoa siku 30 za mwisho
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa
Madini Mhe. Anjellah Kairuki ametoa siku 30 za mwisho kwa mgodi wa GGM
kuhakikisha unawalipa fidia wakazi wa mitaa ya Katoma na Nyamalengo mkoani
Geita ambao nyumba zao takribani 800 zimepata nyufa kutokana na milipuko ya
mgodi huo.
Mhe. Kairuki
ametoa kauli hiyo jana Septemba 30, 2018 wakati akizungumza kwenye kilele cha Maonesho
ya Teknolojia ya Uzalishaji Dhahabu kwa Maendeleo ya Kijamii na Uchumi wa
Viwanda mkoani Geita.
Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki (kulia), akiteta jambo na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Mwl. Doto Biteko (kushoto).
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Viwanda nchini TANTRADE, Edwin Rutageruka (kulia), Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wachimbaji madini FEMATA, John Bina (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Geita wakifuatilia maonesho hayo.
Mgeni rasmi, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Tazama hapa chini BMG Online Tv
SOMA>>>Waziri Mkuu afunga Maonesho ya Teknolojia ya Dhahabu Geita
No comments: